Language

Thursday 28 February 2013

HABARI MUHIMU: TABIBU ALIYEMTOA MIMBA BAAMEDI KUPANDISHWA KIZIMBANI

POLISI Bunda wamesema watamfikisha mahakamani wakati wowote Ofisa tabibu mmoja wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda, anayetuhumiwa kumtoa mimba mhudumu mmoja wa baa ambaye kwa sasa hali yake ni mbaya.

Ofisa tabibu huyo Michael Musimu, ambaye amekuwa akifanya kazi katika kituo cha afya Manyamanya, kilichoko Bunda, anashikiliwa na polisi akituhumiwa kumtoa mimba  mhudumu mmoja wa baa ijulikanayo kwa jina la Savana, iliyoko mjini hapa.
Polisi wamemtaja mhudumu huyo kuwa ni Salome Saimon Bugunda, ambaye sasa hali yake ni mbaya na amepelekwa katika Hospitali ya Rufaa Bugando Mwanza kwa matibabu zaidi.
Imedaiwa kuwa tukio hilo lilitokea juzi na kwamba baada ya Musimu kumtoa mimba mhudumu huyo, hali yake ilibadilika na kumpeleka katika kituo cha afya Manyamanya, lakini hali yake ilizidi kuwa mbaya zaidi na ndipo akakimbizwa katika hospitali ya DDH Bunda ambako pia alipewa rufaa ya kwenda Bugando.
Aidha, imeelezwa kuwa mhudumu huyo ameumizwa vibaya kwani sehemu ya utumbo wake umetoka nje.
Kukamatwa kwa ofisa tabibu huyo kumetokana na mwanamke huyo kumtaja bayana kwa kuwaambia ndugu zake ambao walitoa taarifa polisi. Licha ya polisi kuthibitisha kuwepo kwa tukio hilo na kumshikilia mtuhumiwa huyo, lakini Kamanda wa Polisi Mara, Kamishina Msaidizi wa Polisi, Absalum Mwakyoma amesema bado hajapatiwa taarifa kamili juu ya tukio hilo na kuahidi kulifuatilia.

HABARI MUHIMU: MAGARI YA ZIMAMOTO YAMETAJWA KUVUSHA MALI ZA WIZI UWANJA WA NDEGE WA JK NYERERE DAR

IMEBAINIKA kuwapo kwa wizi wa kutisha katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam, huku magari ya Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji yakitajwa kwamba yamekuwa yakivusha vifaa vya wizi kutoka ndani ya uwanja huo.

Wizi huo ambao umewasababishia hasara kubwa baadhi ya wasafiri wakiwamo wafanyabiashara, abiria wa kawaida na watalii wanaoingia nchini, unadaiwa kufanywa na baadhi ya wafanyakazi wa Wakala wa Mizigo wa Kampuni ya Swissport.
Wafanyakazi hao wamekuwa wakiiba vifaa na bidhaa kwa kuchana mabegi ya abiria kisha kuviweka kwenye makoti yao ya kazi lakini kwa mizigo mikubwa, wamekuwa wakiificha kwenye magari ya zimamoto ambayo huingia na kutoka ndani ya uwanja wa ndege bila kufanyiwa ukaguzi.

HABARI MUHIMU: ZAIDI YA DOLA 377,000 ZIMETUMIKA KUNUNUA IPAD BUNGENI


BUNGE nchini Uganda limetumia zaidi ya dola 377,000 kununa kompyuta aina ya iPad kwa ajili ya wabunge wote .

Maofisa wa bunge hilo walisema kuwa mbali na kuwaweka wabunge hao karibu na ulimwengu wa teknolojia, wanatarajia kuwasaidia kupunguza gharama za fedha zinazotokana na matumizi ya uchapishaji wa nyaraka mbalimbali.
Kamishna wa bunge hilo Elijah Okupa alisema kuwa kompyuta hizo ni bora na zinafaa kwa matumizi hivyo ni vyema zikatumiwa vizuri.
Alisema iPad hizo zitakuwa ni mali ya wabunge lakini kama mtu atatumia kwa muda wa miaka mitano asitegemee itakuwa na ubora uleule wa kumwezesha mwingine atumie kwa miaka hiyo alisema Okupa
Kwa mujibu wa takwimu kutoka katika bunge hilo zilionyesha Serikali imekuwa ikitumia zaidi ya dola 12 katika miaka miwili sasa kwa ajili ya mahitaji ya kama kompyuta, uchapishaji wa nyaraka, mbalimbali kwa ajili ya kuwezesha mawasiliano kuwa bora katika bunge.
Kwa mujibu wa mbunge kutoka mashariki, Medard Segona alisema kuwa kutokana na uwepo wa ipad hizo wanategemea kupunguza matumizi ya fedha zilizokuwa zikipotea hapo awali.
‘’Vifaa hivyo vitapunguza sana matumizi ya fedha kwa kuwa hapo awali wizara ya fedha ilikuwa ikichapisha zaidi ya nyaraka 400 kwa kila mbunge na maofisa wengine waliopo ndani ya bunge hilo’’alisema
Aliongeza kuwa komputa hizo ni muhimu kwa utendaji kazi hasa katika kipindi hicho cha kuendeleza matumizi ya teknolojia.
Hata hivyo taarifa zilisema kuwa wabunge hao bado hawana uelewa mzuri juu ya matumizi hayo licha ya kuwa kampuni imeahidi kutoa mkataba wa mafunzo ambayo pia yatasaidia kupunguza gharama za matumizi.

Wednesday 27 February 2013

HABARI MUHIMU: MTANZANIA AULA RWANDA, APEWA UWAZIRI

RAIS Paul Kagame wa Rwanda amemteua Mtanzania, Profesa Silas Rwakabamba kuwa Waziri wa Miundombinu wa nchi hiyo katika mabadiliko ya Baraza la Mawaziri yaliyofanyika Jumatatu iliyopita.


Kabla ya uteuzi huo, Profesa Rwakabamba alikuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Rwanda. Ni mmoja wa mawaziri wanaoingiza sura mpya katika Baraza la Rais Kagame ambalo amelifanyia mabadiliko kwa kuunda wizara nyingine mpya.

Sura nyingine mpya katika Baraza hilo ambalo liliapishwa juzi Ikulu ya Rwanda ni pamoja na Seraphine Mukantabana (Wakimbizi na Menejimenti ya Maafa) na Oda Gasinzigwa (Ofisi ya Waziri Mkuu- Familia na Jinsia).
Akizungumza kwa simu na mwandishi wetu jana, mdogo wa Profesa Rwakabamba, Timothy Rwamushaija anayeishi Dar es Salaam, alisema ndugu yake alizaliwa katika Kijiji cha Bushagara, Wilaya ya Muleba mkoani Kagera.

HABARI PICHA: UWANJA WA NANE NANE MBEYA WAGEUKA PORI



HABARI MUHIMU: LOWASA ASEMA HOJA YA AJIRA ITAIPA USHINDI CCM

Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, amesema kuwa iwapo serikali zote mbili; ile ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ya Zanzibar, zitatekeleza kwa usahihi maelekezo ya mkutano mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) juu ya suala la ajira, chama hicho kitashinda kiurahisi katika uchaguzi mkuu wa 2015.



Akizungumza kuhusu uchaguzi wa Kenya, Lowassa alisema amefurahishwa na jinsi Wakenya walivyolichukulia tatizo la ajira kama moja ya ajenda muhimu katika uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika wiki ijayo.

Alisisitiza kuwa, kama CCM nayo italichukua tatizo la

KIBONZO


BURUDANI: ALICIA KEYS-GIRL ON FIRE LYRICS

Alicia Keys
Girl On Fire lyrics

Songwriters: Augello-Cook, Alicia J / Remi, Salaam / Bhasker, Jeff

[Alicia Keys]
She's just a girl and she's on fire
Hotter than a fantasy, longer like a highway
She's living in a world and it's on fire
Fill with catastrophe, but she know she can fly away

HABARI MUHIMU: WANNE WANASHIKILIWA NA POLISI KWA KOSA LA KUKUTWA NA KADI 150 ZA ATM NA MILIONI 20 ZA WIZI RUNGWE

JESHI la Polisi Wilaya ya Rungwe, mkoani Mbeya, linawashikilia watu wanne kwa kosa la kukutwa wakitoa fedha kwenye mashine ya (ATM), inayomilikiwa na Benki ya NMB, mjini Tukuyu.


Watu hao walikutwa na kadi 150 za watu tofauti pamoja fedha taslimu zaidi ya sh. milioni 20 walizotoa katika mashine ya ATM, iliyopo karibu na Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya.
Habari zilizolifikia gazeti hili, zinasema wahusika wa wizi huo wamefahamika kwa majina ya Bw. Miraji Kipale (34), Bw. Joseph Peter (20) na Bw. Juma Kabero (20), wote wakazi wa Tukuyu.
Mwingine ni Bw. Jumanne Mgere (29), ambaye ni mkazi wa Mbozi, ambao kati kadi walizokamatwa nazo, 136 tayari walizitumia kuchukua fedha katika ATM.
Habari zaidi zinazongeza kuwa, Bw. Kipale anamiliki ofisi ambayo inaitwa “Nyarusi”, ambayo imekuwa ikitoa mikopo ya fedha kwa watu mbalimbali wakiwemo watumishi wa Serikali hasa walimu
na kurudisha mkopo kwa riba.
Baadhi ya wakopaji, wanadaiwa kuweka bondi vitu mbalimbali vya thamani pamoja na kadi zao za benki (ATM). Watuhumiwa hao pia walikutwa na orodha na majina ya watu 150 pamoja na namba zao za

GAZETI LA RISASI LA LEO


MITINDO: HII STYLE GANI YA KIATU?


HABARI MUHIMU: PAPA BANEDICT WA 16 AAGWA NA WAUMINI ROMA

Waumini kutoka Bavaria,wakishirikiana na wenzao kutoka kila pembe ya dunia wamuaga kiongozi wa kanisa katoliki ulimwenguni
Kiongozi wa kanisa katoliki ulimwenguni, Papa Benedikt wa 16 atakaestaafu kuanzia february 28 na kujishughulisha zaidi na ibada na kutafakari,anaongoza misa yake ya mwisho katika uwanja wa Mtakatifu Petro,wakihudhuria zaidi ya waumini laki moja na nusu kutoka kila pembe ya dunia.Wakaazi wa jimbo la kusini mwa Ujerumani Bavaria anakotokea kiongozi huyo wa kanisa katoliki ulimwenguni wamekuja kwa wingi kumuwaga jamaa yao.
Katika misa yake hiyo ya mwisho ya hadhara kama kiongozi wa kanisa katoliki ulimwenguni,Papa Benedikt wa 16 akiwa ndani ya gari maalum la Vatikan anawaamkia umati wa waumini waliojazana katika uwanja wa Mtakatifu Petro,muda mrefu zaidi kuliko kawaida yake kabla ya kuwakaribisha kwa mazungumzo baadhi ya

MICHEZO: RATIBA YA MECHI ZOTE KUBWA ZA LEO 27/02/2013


HABARI MUHIMU: WANAJESHI WA MAREKANI WAKUBALI KOSA LA KUBAKA

Wanajeshi wa jeshi la wanamaji la Marekani, wamekubali mashtaka ya kumbaka mwanamke mmoja katika kesi ambayo imeibua hisia kali dhidi ya Marekani.


Wanaume hao. Wal;imvamia mwanamke huyo, wakati wa ziara yao fupi katika kisiwa cha Okinawa, makao kwa kambi kubwa ya jeshi la Marekani barani Asia.
Sheria ya kutotoka nje iliyowekewa wanajeshi karibu elfu hamsini kufuatia tukio hilo Okotoba mwaka jana
Kumekuwa na hali ya wasiwasi kati ya majeshi ya Marekani na wenyeji wa Okinawa.
Manamo mwaka 1995, genge la wanajeshi wa Ulaya, lilimvamia na kumbaka msichana mwenye umri wa miaka 12 na kuzua maandamano makubwa.

KAMA HUKUZIPATA BASI HIZI NDIO PICHA ZA UTUPU ZILIZOPIGWA NA WANACHUO WA SAUT



 

HABARI MUHIMU: VITUO VIWILI VYA RADIO VIMEFUNGIWA NA CLOUDS FM IMELIMWA FAINI YA TSH. 5000,000

KAMATI ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetoa adhabu ya kuvifungia muda wa miezi sita vituo viwili vya redio za dini, Imani na Kwa Neema kwa kile kilichoelezwa ni kuendesha vipindi vya uchochezi.

Vilevile kamati hiyo imetoa adhabu ya faini ya Sh5 milioni kwa Kituo cha redio cha Clouds FM baada ya kubainika pia kukiuka taratibu za utangazaji kwa kurusha hewani kipindi kilichotafsiriwa kuwa ni cha uchochezi.
Kamati hiyo ya maudhui ilitangaza adhabu hizo jana jijini Dar es Salaam mbele ya waandishi wa habari ikisisitiza kuwa lengo lao ni kuhakikisha kuwa vyombo vya habari vinazingatia maadili.

Tuesday 26 February 2013

HABARI MUHIMU: DR. SLAA BADO TISHIO

WAKATI baadhi ya wanasiasa wakiwa wameanza kujiwinda kwa ajili ya kuwania urais katika Uchaguzi Mkuu wa 2015, Shirika la Utafiti la Synovate limetoa matokeo ya utafiti wake ambao unaonyesha vigogo tisa kuwamo katika mchuano huo. 

Utafiti huo umeonyesha kuwa endapo uchaguzi huo ungefanyika sasa, Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Willibrod Slaa angeibuka mshindi baada ya kuongoza orodha hiyo akipata asilimia 17. 

Katika matokeo ya utafiti huo uliofanywa Desemba mwaka jana, Dk Slaa anafuatiwa kwa mbali na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ambaye amefungana na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe kila mmoja akipata asilimia tisa.
Hata hivyo, licha ya kuongoza, Dk Slaa ameporomoka kwa asilimia 25 ikilinganishwa na matokeo ya utafiti kama huo uliofanywa na taasisi hiyo mwaka

KUTOKA KATIKA IN BOX YA SIMU YANGU

"Tahadhari...Kundi la waislamu toka Dar es salaam tayari limewasili mikoani kwa ajili ya kuja kubomoa na kuchoma makanisa. Tunatakiwa kuwa makini tuwapo makanisani hata katika kazi zetu. Usipuuze, ni taarifa toka jimbo kuu la Dar es salaam. Wajulishe mapadri, watawa, makatekista, wachungaji, wainjilisti na wakristo wote...nakutakia asubuhi njema na MUNGU akubariki"

Monday 25 February 2013

HABARI MUHIMU: WAGOMBEA WA KENYA KATIKA MDAHALO TENA

Wakenya watakwenda kupiga kura hapo Machi 4 kumchagua kiongozi atakayeiongoza nchi hiyo. Wagombea wa kiti cha urais watafanya mjadala wa

MICHEZO: MSIMAMO WA LIGI KUU UINGEREZA


MICHEZO: RATIBA YA MECHI KUWA ZA LEO IKO HAPA


MICHEZO: MATOKEO YOTE YA MECHI KUBWA ZA JANA YAKO HAPA


MICHEZO:NIYONZIMA"TUTALIPA KISASI KWA KAGERA SUGAR

KIUNGO wa Yanga, Haruna Hakizimana Fadhil Niyonzima, amesema kwamba watalipa kisasi cha kufungwa 1-0 na Kagera Sugar wakati watakaporudiana na timu hiyo kesho, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Akizungumza na BIN ZUBEIRY jana, Niyonzima alisema kwamba wamepania kushinda mechi zote zilizobaki za Ligi Kuu ili kuchukua ubingwa kwa heshima kubwa.
Amesema kwanza lazima walipe kisasi cha kufungwa na Kagera katika mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu, mwaka jana Uwanja wa Kaitaba, Bukoba.
“Kagera walitufunga Bukoba, na sisi lazima tuwafunge hapa Jumatano. Lakini kikubwa ni kampeni yetu ya kushinda kila mechi ili tuchukue ubingwa kwa heshima kubwa,”alisema.
Nahodha huyo wa timu ya taifa ya Rwanda, alisema

HABARI PICHA: HII NDIO NYUMBA YA DIAMOND PLATNUMZ INAYOTARAJIWA KUGHARIMU KIASI CHA MILIONI 260 MPAKA KUKAMILIKA



HABARI MUHIMU: ANALOJIA KUZIMWA MWANZA FEBRUARI 28

MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imesema inatarajia kuzima matangazo ya mfumo wa analojia mkoani hapa Februari 28, mwaka huu, hivyo kuwataka wananchi kuchangamkia fursa ya kujiunga na mfumo mpya wa utangazaji wa dijitali.


Mkurugenzi wa Utangazaji wa TCRA, Habbi Gunze, alibainisha hayo jana alipozungumza na waandishi wa habari mjini hapa.


Alisema matangazo rasmi ya mfumo wa dijitali mkoani hapa Machi mosi mwaka huu, na kwamba TCRA ipo kwenye mchakamchaka wa kutekeleza mipango yake ya makubaliano na nchi nyingine za Afrika Mashariki katika suala zima la kujiunga na mfumo wa dijitali.

VICHWA VYA HABARI VILIVYOBEBWA NA GAZETI LA CHAMPION


HABARI MUHIMU: PADRI WA UINGEREZA ALIYEJIUZULU KISA KASHFA YA NGONO HUYU HAPA

Mmoja wa mapadre waandamizi wa kanisa katoliki nchini Uingereza amejiuzulu wadhifa wake kufuatia shutma za kwamba alikwenda kinyume na matakwa ya kipadre mapema miaka ya themanini.
Kardinal Keith O'Brien ameachia madaraka kama kiongozi mkuu wa kanisa katoliki nchini Scotland na hatarajii kusafiri kwenda Vatican baadaye mwaka huu kumchagua Papa ajaye baada ya baba Mtakatifu Benedict wa 16 kijuzuru.
Inaarifiwa Padre O'Brien aliwauvinjia heshima makasisi mingo mitatu iliyopita.

HABARI MUHIMU: HUU NDIO MTANDAO WA UJAMBAZI MBEYA DAR ES SALAAM, IRINGA NA MOROGORO

POLISI mkoani Mbeya kwa kushirikiana na polisi mkoani Iringa wamegundua mtandao wa majambazi Sugu ambao umekuwa ukihusika na matukio ya mauaji na unyang’aji wa kutumia silaha. 


 Kamanda wa polisi mkoani hapa Diwan Athumani amesem leo(Feb 25) kuwa watu 13 wakiwemo askari wawili wanashikiliwa huku wengine 16 wakiendelea kufanyiwa uchunguzi na jeshi hilo. Kamanda Athumani aliwataja askari waliokamatwa kuhusika na mtandao huo kuwa ni MT 85393 Samwel Balumwina(31) wa kikosi cha 844 KJ cha Jeshi la kujenga Taifa(JKT) Mbeya na polisi G 9101 PC Samwel Kigunye(27) wa kikosi cha kutuliza ghasia(FFU) Mbeya. Alisema askari hao wamekuwa wakihusika na mtandao wa ujambazi kwa kuazimisha sare za polisi na jeshi la wananchi(JWTZ) kwa wenzao wanaokwenda katika matukio ya uvamizi na kusisitiza kuwa

Tuesday 19 February 2013

MICHEZO: MECHI MBALI MBALI ZA LEO


RIPOTI MAALUMU YA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2012-2013

MATOKEO ya mtihani wa kidato cha nne uliofanyika mwaka jana yametangazwa. Watahiniwa 240,903 sawa na asilimia 60.6 wamepata sifuri, huku wanafunzi 23,520 tu ambao ni sawa na asilimia 5.16 ndiyo waliofaulu na wengine 103,327 sawa na asilimia 26.02 wamepata daraja la nne.
Akitangaza matokeo hayo jana, Waziri wa Elimu Dk Shukuru Kawambwa alisema watahiniwa walikuwa 456,137, wa shule wakiwa 397,136 huku wa kujitegemea wakiwa 68,806.
Matokeo ya mwaka huu yamekuwa mabaya sana, Serikali tunasikitika kutokana na hali hii lakini tuna mipango mbalimbali ya kuhakikisha tunaweza kutatua hili tatizo,” alisema Dk Kawambwa.
Dk Kawambwa alisema watahiniwa wote kwa ujumla waliosajiliwa walikuwa 480,036 kati yao wasichana 217,583 sawa na asilimia 45.33 na wavulana 262,453 sawa na asilimia 54.67 lakini waliofanya mtihani huo ni 456,137 sawa na

Wednesday 13 February 2013

MICHEZO: HILI NDILO BASI LILILOTOLEWA NA TBL MAALUMU KWA TIMU YA TAIFA STARS



HABARI MUHIMU: AHUKUMIWA KUNYONGWA HADI KUFA MBEYA

Mahakama kuu kanda ya Mbeya imemhukumu PETER MWAFRIKA mkazi wa Ndolezi wilayani Mbozi kunyongwa hadi kufa baada ya kupatikana na hatia ya kuua kwa kukusudia.



Akisoma hukumu hiyo iliyochukua saa 1.30 Jaji mfawidhi wa mahakama kuu kanda ya mbeya NOEL CHOCHA amesema licha ya mikono ya mahakama kufungwa kutoa adhabu ndogo kwa kosa la maauaji ya kukusudia, pia adhabu hiyo ni hatua ya kukomesha watu wenye tabia kama za mtuhumiwa kujichukulia hatua mikononi mwao.
Akirejea mazingira ya kesi hiyo jaji Chocha amesema mnamo Februaly 11,2010 Mshatakiwa na wenzake watatu walifanya kosa la mauaji ya kukudia chini ya kifungu 196 chasheria ya

mwenendo wa makosa ya jinai kwa kumuua KOSAM MWAFRIKA ambaye ni kaka wa marehemu katika kijiji cha Shaji kwa kumkata koromeo na kulitenganisha vipande viwili.
Jaji Chocha katika maelezo yake alisema mshtakiwa akiwa na wenzake ambao walitoweka baada ya mauaji hayo walimvamia Kosam akiwa na mkewe shambani

MICHEZO: MATOKEO NA RATIBA YA MECHI KUBWA ZA LEO DUNIANI


HABARI PICHA: MGAWANYIKO UNASHIKA KASI TANZANIA, HIZI NDIO BUTCHER ZA WAKRISTO


HABARI MUHIMU TOKA GPL: FREEMASONS WAUTEKA MJI WA MOSHI

IMANI ya jamii ya siri ya Freemasons imeonekana kuuteka Mji wa Moshi na vitongoji vyake kutokana na matangazo mengi kubandikwa kila kona yakihamasisha wafuasi kujiunga huku ofa ya utajiri ikipewa kipaumbele.

Risasi Mchanganyiko limeshuhudia matangazo mengi yanayohamasisha kujiunga na imani hiyo yakiwa yamebandikwa kila kona ya mji huu ikiwemo katika nguzo za umeme
Katika tangazo hilo, wahusika wameeleza kwamba watakaojiunga mapema watapewa magari ya kifahari na nyumba za kisasa ikiwa ndiyo njia za awali za kubadilisha maisha yao.
Mwandishi wetu alijifanya anataka kujiunga na kupiga namba za simu zilizowekwa katika tangazo hilo ambazo ni 0783 127 967 ambapo ilipokelewa na mwanaume aliyekataa kutaja jina lake lakini alitoa masharti ya kujiunga.
“Tuma majina yako matatu; lako, baba na babu yako halafu tuma na shilingi 100,000 kwenye namba 0714 084 841 ambayo ni ada ya uanachama kisha utakwenda Kindoroko Hotel, chumba namba 87 hapo utakutana na bosi wangu na utaandikishwa rasmi na kupewa nguo zenye nembo yetu,” alisema mtu huyo.

Mwandishi wetu alifika katika Hoteli ya Kindoroko iliyopo mjini hapa juzi, Jumapili Februari 10, mwaka huu, akaonana na mtu wa mapokezi na kujitambulisha kama mwanachama mpya anayetaka kuonana na mhusika aliyepanga chumba namba 87.
Cha kushangaza, mhudumu alimwambia hawana mteja wa aina hiyo katika hoteli yao na kwamba hakuna chumba chenye namba aliyoelekezwa, jambo lililoonesha wazi kuwa wahusika ni matapeli wanaotaka kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu.
Naye meneja wa hoteli hiyo aliyejitambulisha kwa jina moja la Sara alipopigiwa simu, alitoa majibu kama ya mtu wa mapokezi.
Upekuzi wa gazeti hili umebaini kuwa, simu namba 0714 084841 iliyotakiwa kutumiwa fedha na mtu aliyejiita wa Freemasons imesajiliwa kwa jina la Flora Tuvana.
 

TAARIFA YA KIFO CHA MSANII WA TMK WANAUME HALISI 'BK'


HABARI MUHIMU-OLE WAO WANAWAKE WAVUTAJI WA SIGARA

Wataalamu wa afya wanasema kuwa wanawake barani Ulaya wanafariki zaidi kutokana na saratani ya mapafu kuliko saratani ya matiti.

 

Wanaelezea kuwa saratani ya mapafu ndio imekuwa sasa saratani nambari moja ambayo inasababisha vifo miongoni mwa wanawake.
Hali hii tayari inashuhidiwa nchini Uingereza na Poland.
Kulingana na watafiti, hii ni ishara ya idadi kubwa ya wanawake wanaovuta sigara hali iliyoanza kujitokeza kuanzia mapema miaka ya tisini na sabaini.
Idadi ya vifo vinavyotokana na saratani ya mapafu, vitaendelea kuongezeka katika miaka ijayo, lakini sasa kwa sababu ya vijana wa kike wasiovutiwa na kuvuta sigara na ambao idadi yao sio kubwa sana , huenda vifo hivyo vikapungua.
Mwaka 2013, takriban wanawake 82,640 barani Ulaya watafariki kutokana na saratani ya mapafu ikilinganishwa na wanawake 88,886 watakaofariki kutokana na saratani ya matiti.
Wanatarajiwa kuwa vifo vinvyotokana na saratani ya mapafu kupungua mwaka 2020 au 2025 kwa sababu angalu vijana wa kiike hawavuti sana sigara.
Lakini ifikapo mwaka 2015, wanawake wengi watafariki kutokana na saratani ya mapafu kuliko saratani ya matiti, kulingana na mtaalamu wa afya ya wanawake, Profesa Carlo La Vecchia .
Takwimu zinaonyesha kuwa ingawa watu wengi zaidi wanaugua saratani, kwa sababu wanaishi muda mrefu zaidi,
ni watu wachache sana wanafariki kutokana na saratani.

Licha ya kupungua kwa idadi ya watu wanaofariki kutokana na saratani barani humo, idadi ya wanawakewanaofariki kutokana na saratani ya mapafu inaongezeka katika nchi zote za Ulaya.
Profesa La Vecchia,wa chuo kikuu cha Milan, Italy, anasema kuwa hali hii inaleta wasiwasi kwa sababu hakuna dalili kuwa ugonjwa huo unapungua.
Uvutaji sigara pamoja na ugonjwa wa sukari ndio vinachangia kuongezeka kwa ugonjwa huu. Lakini wataalamu wanasema bado hawajui nini kinasababisha sehemu kubwa ya saratani hiyo.
Wataalamu wanasema kuna umuhimu wa wanawake kuwacha kuvuta sigara

BURUDANI: N'SYNC-THIS I PROMISE LYRICS

"This I Promise You"
Ohh ohh...

When the visions around you,
Bring tears to your eyes
And all that surround you,
Are secrets and lies
I'll be your strength,
I'll give you hope,

BURUDANI: TID NAYE KWENDA BIG BROTHER AFRICA



Baada ya jana kusikia kuwa q chifu kachukua form TID nayeye naye kachukua form ya kushiriki big brother  na kufiksha idadi ya wasanii wa ongo kuwekahistoria ya kuchukua form za big brother ambako wema sepetu na nyeye aliichukua q cheaf na hemed pia wato kwenye nia ya kubeba kitita cha dola za kimarekani 300,000
Mshiriki wa mwaka jana Julio aliongea nakusema mtu kama TID angefaa sana kushiriki shindano hilo maana ni mcheshi na ana vigezo vingi vitavyomuwezesha kushinda.

BURUDANI: KUNDI LA MUZIKI LA PAH ONE LAMONG'ONYOKA!!!

Kundi ambalo lilikuwa linaundwa wasanii wanne kwa pamoja likiitwa Pah One sasa limevunjika kwani First Lady wa kundi hilo la Pah One mwanadada Aika ametangaza kujitoa rasmi kwenye kundi hilo pamoja na rapper na producer wa kundi hilo Nahreel na hivyo kundi hilo kubakiwa na wasanii wawili tu. Aika amesema kuwa sababu ya kumfanya ajitoe kwenye kundi hilo ni kutokuwa na maelewano mazuri ndani ya kundi hilo na kuongeza kwa kusema Nahreel ni Solo Artist hivyo yeye na Nahreel hawajavunja kundi hilo na si kwamba mapenzi yake yeye na Nahreel ndiyo sababu iliyopelekea kuvunjika kwa kundi hilo. Nahreel na Aika wanatarajia kuachia ngoma yao ya kwanza wakiwa kama Solo Artists tarehe 14 mwezi huu.

KIBONZO


HABARI MUHIMU: WIFI ANG'ATWA ULIMI MPAKA KUKATIKA

MWALIMU wa Shule ya Msingi Mfaranyaki iliyopo Manispaa ya Songea, Theresia Fuli anashikiliwa na polisi kwa kosa la kumjeruhi kwa kumng’ata ulimi hadi kukatika wifi yake kwa wivu wa mapenzi.

Akizungumza kwa tabu na gazeti hili jana kwenye hospitali ya mkoa alikolazwa wodi daraja la kwanza kwa ajili ya matibabu, majeruhi huyo Oliga Msigale mkazi wa Msamala amesema, bado ana maumivu makali ya ulimi ingawa amepatiwa matibabu.
Amesema siku ya tukio alishangaa kuona anavamiwa na wifi yake ambaye ni mtalaka wa kaka yake, ambapo alimtupia mtoto mkubwa wa kaka yake maharage ya moto kisha kumvamia yeye, huku akimtuhumu kuwa ndiye binti ambaye amechukua nafasi yake bila kujua kuwa yeye ni ndugu wa mume na alipoanguka chini alikabwa koo na alipotoa ulimi nje mwanamke huyo bila huruma alimngata ulimi na kutoa kipande cha ulimi kisha akatoroka eneo hilo.

Tuesday 12 February 2013

HABARI MUHIMU: POLISI KUWASAKA WOTE WANAOMTUKANA ANNE MAKINDA

POLISI mkoani Dar es Salaam wametangaza kuwafuatilia, kuwasaka na kuwachukulia hatua wote waliotuma ujumbe wa matusi ama kupiga simu ya vitisho kwa Spika wa Bunge, Anne Makinda.

Viongozi wa Chadema walifanya mkutano wao mwishoni mwa wiki kwenye Viwanja vya Mwembe Yanga, Temeke, jijini Dar es Salaam na kutoa namba za Spika wa Bunge ili mashabiki wamshinikize ajiuzulu.
Pia viongozi hao walitoa namba za simu za Naibu Spika, Job Ndugai ili naye ashinikizwe ang’oke katika nafasi yake kwa madai ya kukandamiza upinzani bungeni.
Chadema walidai kuwa Makinda na Ndugai
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...