Language

Monday 14 January 2013

HABARI: VIFO VYA MAMA NA MTOTO SAS BASI


MAKAMU wa Rais Dkt. Mohamed Gharib Bilal, leo anafungua mkutano wa kimataifa wa Afya ya Mama ambao utahusisha washiriki kutoka zaidi ya nchi 68 wakiwemo wanasiasa.


Akizungumza na waandishi wa habari mjini Arusha jana, Mkurugenzi wa Asasi ya Management and Development for Health (MDH), Dkt. Chalamila Guerino, alisema mkutano huo utakuwa na manufaa kwa afya ya wanawake wajawazito ambao kila siku wanapoteza maisha wakati wa kujifungua.Alisema mkutano huo utakuwa wa siku tatu, utajadili changamoto mbalimbali wanazopata wajawazito kwenye uzazi na utafungwa Januari 17 mwaka huu na Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete.“Mkutanio huu utakuwa na washiriki wasiopungua 700, wakiwemo wanasiasa ambao watapewa mbinu mbalimbali zitakazowasaidia kujua masuala ya afya ya mama ili kupunguza vifo vinavyotokea.“Wanasiasa watapewa mbinu na elimu ya kuzungumza na wananchi ili jamii iweze kuepukana na vifo vinavyochangia umaskini nchini,” alisema Dkt. Guerino.Akizungumzia vifo vya wajawazito hasa wakati wa kujifungua, alisema Tanzania bado inakabiliwa na changamoto hasa maeneo ya mijini ambayo vifo ni vingi.“Takwimu za kidunia nazo zinaonesha kuwa, asilimia kubwa ya wanawake wanapoteza maisha hasa wakati wa kujifungua, nchini Tanzania wanawake 454, kati ya 100,000 hufariki dunia wakati wa uzazi huku.“Kwa nchi zinaendelea duniani, wanawake 300,000 hufariki dunia hivyo tunapaswa kupambana na hali hii haraka kwa kuhusisha makundi mbalimbali pamoja na wanasiasa,” alisema.Alisema kwa upande wa mijini nchini, changamoto bado ni nyingi ambapo ili vifo hivyo viweze kuwa historia, lazima tuwe na umoja ambao ni thabiti ili kuokoa maisha ya wanawake.Aliongeza kuwa, mkutano huo pia utajadili upatikanaji wa vitendea kazi ili kuboresha huduma ya afya kwa wajawazito na upimaji ubora ambapo kupitia mada hizo, Tanzania itaweza kuepusha vifo vingi vya wanawake wajawazito.

BURUDANI: JOKATE 'KIDOTI' KUOLEWA MWAKA HUU?

Miss Temeke 2006/07, Jokate Mwegelo 'Kidoti' anadaiwa kuchumbiwa kwa siri nyumbani kwao, Songea mkoani Ruvuma alipokwenda kusherehekea Sikukuu ya Mwaka Mpya.
Kwa mujibu wa mtu wa karibu wa staa huyo, Jokate alitimba Songea akiongozana na rafiki zake wawili pamoja na baadhi ya ndugu.
Chanzo hicho kilidai kuwa kilipochunguza amekwenda kufanya nini mkoani humo, ndipo ikabainika kuwa alikwenda kusherehekea Mwaka Mpya akiongozana na wazazi wake anaoishi nao Dar, lengo likiwa kukamilisha mambo ya mila kwani alikuwa ameposwa na mchumba ambaye hakutajwa.
Mtu huyo aliendelea kudai kuwa nyumbani kwa akina Jokate ambaye aliapa kuwa lazima mwaka huu aolewe, kulikuwa na wageni wengi ambao miongoni mwao ndiyo waliopeleka posa.
Baada ya habari hizi kutua mezani,mwandishi wetu aliongea na Jokate kwa njia ya simu ambaye alikiri kwenda kwao Songea lakini hakutaka kudadavua ishu ya kuchumbiwa.
“Mh! Watu ni wambeya jamani! Mimi nilienda kwetu na ninatarajia kufanya kitu kikubwa huko Songea mtakisikia ‘soon’,” alisema Jokate huku akicheka.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...