Language

Tuesday 15 January 2013

HABARI PICHA: NDOA ZA JINSIA MOJA ZINAZIDI KUSHIKA KASI AFRIKA


HABARI: KIGOGO WA CCM MSAGAJI HUYU HAPA

Mwenyekiti wa CCM, Tawi la Washington DC, Marekani, Loveness Mamuya, yupo kwenye uhasama mkali na Mtanzania mwenzake anayeishi nchini humo, Linda Bezuidenhout, kiasi cha kuchafuana na kuibua aibu nzito.

Loveness

Rekodi zinaonesha kuwa Loveness na Linda walikuwa marafiki wakubwa lakini kwa sasa ni maadui wasiopikika chungu kimoja, huku mitandao ya kijamii, hususan Facebook na skendo ya usagaji, vikitajatajwa katika malumbano yao.
Baada ya malumbano na kuchafuana, wiki iliyopita mwandishi wetu aliwapata mahasimu hao, akarekodi sauti zao ambapo kila mmoja alitoa ya moyoni kuhusu mwenzake.
ALICHOKISEMA LINDA

Linda

Linda ambaye ni dada wa mshindi wa Big Brother Africa mwaka 2007, Richard Bezuidenhout alidai: “Tatizo kubwa la Loveness ni usagaji. Miaka saba iliyopita wakati naishi Maryland (Marekani), nilikuwa na matatizo ya nyumba. Nilikuwa sina hati za kuniwezesha kupanga nyumba yangu mwenyewe.
“Nikawa nachangia nyumba na watu wa nchi nyingine, nanyanyasika, tunagombana. Loveness akasikia matatizo yangu, akanipigia simu. Akaniambia ananijua tangu nikiwa Dar es Salaam. Baadaye akanishawishi nihamie kwake halafu atanisaidia kupata hati niweze kupata nyumba niishi mwenyewe na watoto wangu. Wakati huo nilikuwa na watoto wawili, mmoja ana miaka sita, mwingine mmoja na nusu.
“Nilipohamia nyumbani kwake, siku zikawa zinakwenda hafuatilii makaratasi yangu wala hataki kujishughulisha kunitafutia nyumba. Kinyume chake akawa ananitongoza tusagane, mimi nikamkatalia, basi akawa ananifuata chumbani usiku, ananilazimisha tufanye huo mchezo wa kusagana.
“Kila siku alikuja chumbani kwangu, mimi nikawa nashindwa kumjibu kwa ukali kwa kuhofia atanifukuza, nikawa nasingizia watoto wangu hawajalala, yeye anasema wamelala, mimi naendelea kumsisitizia hawajalala kwa sababu mimi ndiye nawajua.
“Siku zikawa zinakwenda, siku moja nikamuuliza ni kwa nini hataki kunisaidia kupata nyumba, au mpaka anifanyie huo mchezo? Hapo nikawa nimemtibua lakini baadaye ikabidi nijifanye nimelainika, akatulia lakini nikaendelea kumkatalia kijanja kunifanyia huo mchezo wake.
“Kuna wakati alinunua mpaka nyeti bandia ya kiume akidhani mimi nitakubali. Vilevile kuna siku alinibaka, hiyo siku siku alinunua pombe tukalewa, nilipolala, katikati ya usingizi nikashtuka kusikia mtu amenilalia.

“Nikamsukuma, kutokana na pombe sikumzingatia, nikaendelea kulala. Asubuhi nikakumbuka lile tukio, nikamuuliza Loveness kama alikuja chumbani kwangu usiku, akanijibu ndiyo na nilimsukuma. Akaniambia pia kwamba hakutaka kuendelea kwa sababu aliponishika aligundua nilikuwa katika siku mbaya.
“Nikajua mambo yamekuwa mazito, kwa hiyo nikamuomba anisaidie kupata nyumba, baada ya hapo, atakuwa anakuja kwangu tunafanya huo mchezo kwa kujiachia. Kusikia hivyo, Loveness akaondoka na mume wake, wakaenda kutafuta nyumba, jioni wakaniambia wamepata.
“Yaani baada ya kumuahidi tutakuwa tunafanya mchezo wake ndiyo akapata nyumba haraka. Nikahamia na watoto wangu. Baada ya hapo, nikamhamishia na mdogo wangu mwingine. Loveness akaona mdogo wangu atakuwa anamfanya asifanikiwe lengo lake la kufanya mchezo wa usagaji na mimi.
“Loveness akanigombanisha na mdogo wangu, akahama lakini baadaye yule mdogo wangu akaja kunipa siri nzima ya maneno ya uchonganishi aliyokuwa anaambiwa na Loveness. Kwa kweli kitendo cha kunigombanisha na mdogo wangu kiliniudhi sana, ikabidi nianike uchafu wote na njama zake za kujidai ananisaidia ili anifanyie mchezo wa usagaji.”

 

LOVENESS NAYE AKAZUNGUMZA
“Mimi Linda alikuwa rafiki yangu, alibadilika tu kwa sababu ya kunionea wivu. Ni uongo mtupu,” alisema Loveness na kuongeza:
“Kiukweli tuligombana kwa vitu tofauti. Alikuwa anaishi kwangu nikamfukuza kutokana na tabia zake lakini nashangaa haya mambo yamekua makubwa hivi sasa.”
SIASA ZATAJWA
Loveness: “Mimi naamini haya maneno ya Linda yamechochewa na siasa. Unajua tangu tufungue tawi la CCM DC, imekuwa tabu sana. Maneno mengi yanazungumzwa. Mfano, mimi na Linda tuligombana karibu miaka saba iliyopita lakini hayakusemwa, nilipofungua tawi la CCM tu ndiyo mambo yakawa makubwa.
“Wakaanzisha mpaka ukurasa wa kikundi Facebook, wakawa wananitukana. Mimi sishangai sana kwa maana Linda ni Chadema damu na mimi ni CCM damu, hizi ni siasa tu.”

BURUDANI: HIZI NDIO PICHA ZILIZOACHA MASWALI KWA WATU 'BAADA YA DIAMOND NI ZAMU YA JB KWA WEMA???'



HABARI: UN YAUNGA MKONO MAJESHI YA UFARANSA MALI

Wanachama wote wa Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa wameunga mkono harakati za jeshi la Ufaransa dhidi ya wapiganaji wa kiisilamu nchini Mali.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon alisema kuwa anatumai hatua ya jeshi hilo itaweza kurejesha utulivu na uthabiti nchini humo.
Ufaransa iliingilia mzozo huo siku ya Ijumaa baada ya wapiganaji kuanza kusonga mbele Kusini mwa nchi.
Maafisa wa utawala nchini Ufaransa, walisema kuwa wanahofia waasi huenda wakaukaribia mji mkuu Bamako na kusababisha tisho kubwa la usalama katika eneo hilo zima.
Siku ya Jumatatu , baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, lilifanya mkutano mjini New York kufuatia ombi la Ufaransa.
Baada ya mkutano, balozi wa Ufaransa katika Umoja wa Mataifa,Gerard Araud alisema kuwa nchi yake inaungwa mkono na wanachama wote wa baraza la usalama.
Lakini aliongeza kuwa Ufaransa pia ilitaka wanajeshi wa nchi za Afrika Magharibi kupelekwa Mali mara moja.
Hatua ya baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kuunga mkono jeshi la Ufaransa ni ishara ya wasiwasi mkubwa uliopo kuhusu uwezo wa makundi ya kiisilamu yaliyojihami nchini Mali.
Wanadiplomasia wanaonekana kuwa na wasiwasi kuhusu kuwasili kwa wanajeshi nchini Mali kusaidia na harakati za jeshi la Mali dhidi ya waasi.

MITINDO: KAMA UNAPENDA KUTUPIA SUIT (SUTI) HII INAKUHUSU ZAIDI








BURUDANI: KAMA ULIKUWA HUJUI LEO NI BIRTHDAY YA PITBULL, NA HIKI NDICHO ALICHO KITWEET KUTOA BAADA YA KUPEWA SALAMU ZA BIRTHDAY YAKE

Born: January 15, 1981 (age 32), Miami
Height: 1.77 m
Full name: Armando Christian PĂ©rez
Nationality: American


MICHEZO: HII NDIO MECHI YA KESHO KATIKA LIGI KUU UINGEREZA


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...