Language

Saturday 19 January 2013

MICHEZO: MATOKEO YA MECHI ZA JANA NA RATIBA YA MECHI ZA LEO LIGI KUU UINGEREZA


MITINDO: UVAAJI WA SKETI FUPI (MINI SKIRT) HUTEGEMEA UMBO LA MVAAJI NA MAZINGIRA






MICHEZO: ARMSTRONG ALILIA KIFUNGO CHAKE CHA KIFO

Mwendeshaji baiskeli Lance Armstrong ameelezea kushangaa kwa kukabidhiwa adhabu ya maisha ya kutoshiriki katika michezo, ilhali wanamichezo wenzake wamekuwa wakipigwa marufuku ya miezi sita tu
 
Katika sehemu ya pili ya mazungumzo yake na Oprah Winfrey, mwanamichezo huyo mwenye umri wa miaka 41 alisema: "Ninastahili kuadhibiwa. Lakini sidhani ninastahili hukumu ya kifo."
"Ningelitamani sana kupata nafasi ya kushindana, lakini hiyo sio sababu ya yale ninayoyafanya."
Kwa usiku wa pili, mazungumzo yake na Winfrey, mwenye umri wa miak 58, yalipeperushwa katika muda ambao watazamaji wengi walipata fursa ya kutizama televisheni, na yalionekana kote duniani kupitia tovuti yake.
Mazungumzo hayo yalikuwa hewani kipitia kituo cha Winfrey cha televisheni nchini Marekani, OWN, yaani Oprah Winfrey Network.
Katika sehemu ya kwanza ya mazungumzo yao, Mmarekani Armstrong hatimaye alikiri kutumia dawa za kuongezea nguvu michezoni zilizopigwa marufuku, baada ya kukanusha kwa muda wa miaka mingi, na huku akiibuka bingwa mara saba wa mashindano ya baiskeli ya Tour de France.

HABARI: WABUNGE 31 WAMEJIANDIKISHA KWENDA JKT

Wabunge vijana katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wameanza kujiandikisha tayari kwa kujiunga na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kwa Mujibu wa Sheria kwa ajili ya mafunzo yatakayoanza Machi mwaka huu.
Taarifa zimeeleza kuwa, idadi ya wabunge ambao tayari wamejiandikisha kujiunga na JKT hadi sasa ni zaidi ya 31, huku wengine wakiendelea.
Kujiandikisha kwa wabunge hao ili wajiunge na JKT kunafuatia wito uliotolewa na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha, Julai mwaka uliopita, alipowasilisha hotuba ya bajeti ya wizara yake katika Bunge la Bajeti mjini Dodoma.
Kwa nyakati tofauti wabunge vijana kutoka CCM, Chadema na NCCR- Mageuzi walilithibitishia gazeti hili kuwa tayari wamejiandikisha katika Ofisi ya Katibu wa Bunge kwa ajili ya mafunzo hayo.
Imebainishwa kuwa, miongoni mwa wabunge waliojiandikisha, wamo pia ambao waliwahi kupitia mafunzo hayo, ikielezwa kuwa wamefanya hivyo wakitaka kwenda kujikumbushia.
Hata hivyo, Kaimu Katibu wa Bunge, Eliakimu Mrema hakuwa tayari kuzungumzia suala hilo akieleza kuwa linaweza kuzungumziwa na Spika wa Bunge kwa kuwa ndiye anayezungumzia masuala ya wabunge.
Sisi kazi yetu ni utendaji tu na masuala ya wabunge, Spika ndiye anayezungumzia,”alisema Mrema.
Alipotakiwa kuzungumzia taarifa hizo, Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai, alisema kwamba ni mapema mno kuzungumzia suala hilo kwa kuwa hawajapata idadi kamili.
Tukiwa Dodoma (bungeni), ukituuliza tutakuwa tayari kutoa taarifa kamili, lakini kwa sasa ni mapema kuzungumzia suala hilo,”alisema Ndugai na kuongeza:
Watu ni rahisi kusema, lakini wakati mwingine utekelezaji ni mgumu kama unavyosema kwani, ukisikia moja ya uamuzi mgumu, hili ni mojawapo.
Ndugai alisema kuwa mafunzo hayo hayatawahusu wabunge ambao waliwahi kupitia JKT siku za nyuma na kwamba ni maalumu kwa wabunge vijana.
Naomba usubiri Dodoma, tutakuambia hali ilivyo,” alisema Ndugai
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...