Language

Friday 25 January 2013

HABARI PICHA/BURUDANI: HAPPY 32 YEARS TO MWANADADA ALICIA KEYS


MICHEZO: LIVESCORES UPDATES YA MECHI ZOTE MPAKA SASA IKO HAPA


BURUDANI: LULU KUENDELEA KUSOTA SELO,NI BAADA YA DHAMANA YAKE KUPIGWA KALENDA

Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imesogeza mbele tarehe ya usikilizwaji wa maombi ya dhamana ya msanii wa fani ya maigizo, Elizabeth Michael, maarufu kama Lulu, anayekabiliwa na kesi ya kuua bila kukusudia.

Lulu aliwasilisha mahakamani hapo maombi ya dhamana, kupitia kwa jopo la mawakili wake linaloongozwa na Wakili Kennedy Fungamtama, Makamu wa

HABARI: KESI YA SISTA ALIYEFUMANIWA NA MUME WA MTU SUMBAWANGA KUSIKILIZWA TAREHE 29

KESI  ya  madai  inayomkabili aliyekuwa  Mtawa wa Shirika la Kitawa la Kanisa Katoliki Jimbo la Sumbawanga, Sista Yasinta Sindani anayedaiwa kufumaniwa na mume wa mtu imepangwa  kusikilizwa Januari 29 mwaka huu.
“Sista’ Yasita  licha ya kuwa mtumishi  wa afya katika  Hospitali ya Mkoa wa Rukwa mjini hapa  lakini inadaiwa  ameachana  na maisha  ya  kitawa  miaka  miwili  iliyopita kwa hiyari yake akiwa Mtawa  wa Shirika la  Masista wa Maria Mtakatifu Malkia wa Afrika (MMMA).
Shauri  hilo  la madai  linatarajiwa  kuanza kusikiliza  katika Mahakama ya Mwanzo mjini hapa, mbele ya Hakimu  Jaffari  Mkinga, mlalamikaji Asteria Mgabo anamtaka Yasinta amlipe Sh3 milioni baada ya kumfumania na mumewe wa ndoa aitwaye  Martin Msangawale (39), Mhasibu wa Manispaa ya  Sumbawanga.
Siku hiyo  ya kusikilizwa kwa shauri  hilo  mlalamikaji  katika  shauri  hilo  Asteria  anatarajiwa  kuwaleta  mashahidi wake  wanne mahakamani hapo

HABARI: SITTA KUGOMBEA URAIS 2015

Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta amesema kwamba anazo sifa za kuwa Rais wa Tanzania na anafikiria kugombea 2015, iwapo dhamira yake itaridhika na mazingira na upepo wa kisiasa wa wakati huo.
Akizungumza katika mahojiano maalumu, Sitta alitaja mambo kadhaa aliyoeleza kuwa ni ishara ya kukubalika kwake, ikiwamo kuteuliwa na marais wote wanne; Julius Nyerere, Ali Hassan Mwinyi, Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete katika nyadhifa mbalimbali ikiwamo ya uwaziri.
Kauli ya Sitta imekuja baada ya kuwapo kwa minong’ono ya baadhi ya wananchi kumtaja kuwa miongoni mwa watu wanaoweza kujitokeza kugombea urais katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2015.
Ni faraja kusikia watu wakinizungumzia kuwa ninazo sifa (za kuwa Rais). Nami ninaamini ninazo sifa. Wakati utakapofika nitajipima. Kama hali hii itaendelea, basi nitaona ni vizuri nigombee,” alisema Sitta ambaye aliwahi kuwa Spika wa

HABARI KUBWA KATIKA MAGAZETI YA LEO: MAKAHABA: HATUTAACHA KUJIUZA NG'O...WAKATI SKENDO CHAFU ZA MASTAA WA FILAMU BONGO ZIMEFIKA KWA JK



BURUDANI: MH. JERRY SLAA MGENI RASMI USIKU WA MASTAA WA FILAMU

Meya wa Ilala Jerry Slaa ndiye atakuwa mgeni rasmi kesho katika Tamasha la Usiku wa Mastaa wa Filamu litakalofanyika katika ukumbi wa kisasa wa burudani Dar Live, Mbagala Zakhem jijini Dar es Salaam. Katika tamasha hilo burudani mbalimbali kutoka kwa wasanii wa filamu na wale wa Bongo Fleva zitakuwepo

HABARI: JESHI KUCHUKUA UONGOZI UGANDA?

Baada ya sakata la kufariki ghafla mbunge wa chama tawala NRM nchini Uganda,rais Museveni pamoja na waziri wa ulinzi na mkuu wa majeshi wamekuwa wakitoa kauli za kutishia kuliachia jeshi lichukue uongozi nchini humo. 

Nchini Uganda baada ya sakata la wiki kadhaa la kufariki ghafla mbunge wa chama tawala NRM na aliyekuwa mkosoaji mkubwa wa serikali ya chama chake inayoongozwa na Museveni Selina Nambanda,sasa rais pamoja na waziri wa ulinzi na mkuu wa majeshi katika nyakati tofauti wamekuwa wakitoa kauli za kutishia kuliachia jeshi lichukue uongozi nchini Uganda. Yote yanatokana na mpasuko ndani ya chama cha NRM ambapo wabunge wa chama hicho wamekuwa wakitaka ianzishwe tume huru ya kuchuguza kifo hicho,hatua ambayo inapingwa na rais Museveni.Wabunge kadhaa wameshatiwa ndani kufuatia hoja hiyo.Kinachowatia wengi mashaka kwa sasa ni kauli hizo za kutaka jeshi liidhibiti serikali, Saumu Mwasimba amemuuliza mchambuzi wa masuala ya kiasiasa,mhadhiri wa masuala ya sheria katika chuo kikuu cha Makerere,Dkt John Nsokwa anaitazama vipi hatua hii. Kusikiliza mazungumzo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.

`MICHEZO: RATIBA YA MECHI ZA LEO KATIKA VIWANJA MBALI MBALI DUNIANI



Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...