Language

Saturday 2 February 2013

HABARI: HII NDIO SIRI YA MGOGORO WA MTWARA

MOJA ya mambo yaliyoamsha hisia za wakazi wa Mkoa wa Mtwara hadi kushinikiza kwa vurugu wakitaka gesi isitoke mkoani humo, ni taarifa kuwa nishati hiyo ingepelekwa wilayani Bagamoyo, nyumbani kwa Rais Jakaya Kikwete.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alisema jana nyumbani kwake mjini Dodoma kuwa, mbali na imani hiyo, amebaini pia kuwa mpasuko ndani ya CCM mkoani Mtwara na harakati za kisiasa ni sababu nyingine iliyochochea mgogoro huo.
Pinda alikuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mgogoro huo ambao ulisababisha vifo vya watu wanne huku wengine wakijeruhiwa vibaya na uharibifu mkubwa wa mali zikiwamo nyumba za wabunge kuchomwa moto na namna alivyofanikiwa kuuzima.
Waziri Mkuu alifanya ziara ya siku mbili mkoani Mtwara, Januari 25 na 26 mwaka huu na kufanikiwa kuzima mgogoro huo baada ya kufanya mazungumzo na makundi mbalimbali ya wadau wa gesi mkoani humo.
“Sasa hili nililitolea ufafanuzi kwa kukanusha kuwa siyo kweli kwamba gesi inakwenda Bagamoyo. Lakini pia baada ya kukaa nao nilibaini kuwa hata viongozi wenyewe wa CCM hawako pamoja,” alisema Pinda na kuongeza:
“Pamoja na hayo nikachukua

HABARI: MTANGAZAJI WA REDIO TZ AMEKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA KENYA

MAMLAKA ya Mapato Kenya(KRA),inamshikilia mwandishi wa habari wa Tanzania kwa tuhuma za kusafirisha dawa za kulevya aina ya heroin kiasi cha kilo 5.436 zenye thamani ya karibu Sh234 milioni.
Mtanzania huyo ambaye aliwahi kuwa mtangazaji katika kituo kimoja cha redio nchini, alikamatwa akiwa anataka kusafirisha dawa hizo kwenda China.
Mamlaka ya Mapato Kenya inataka kutaarifu maendeleo ya sakata la kukamatwa kwa kilo 5.436 za heroin zilizokamatwa Januari 23 mwaka 2013 saa 4:40 usiku.”
Imethibitika kuwa kilichokamatwa ni dawa aina ya heroin yenye thamani ya Sh13 milioni za Kenya…kwamba mtuhumiwa… (Jina tunalo kwa kuwa hajafikishwa mahakamani) hakuwa mwanafunzi lakini ni mtangazaji wa redio nchini Tanzania.”
Ametambulika kuwa mtangazaji wa kituo kimoja cha redio kwa tuhuma za kusafirisha dawa za kulevya aina ya heroin zenye thamani ya
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...