Language

Sunday 5 May 2013

KAMA UNAFUATILIA MPIRA WA SPAIN, HIZI NDIO MECHI ZITAKAZOCHEZWA KATIKA VIWANJA VYAO LEO MAY 5


RATIBA YA MECHI KALI ZA LEO ENGLAND


DOWNLOAD HAPA WIMBO MPYA WA AY NA FID Q-JIPE SHAVU

JINSI BASI LA TAQWA LILIVYOUWA 7 NA KUJERUHI VIBAYA ZAIDI YA 20 IRINGA


Abiria saba waliokuwa wakisafiri na basi la kampuni ya Taqwa lenye namba za usajili T 273 CDR kutoka jijini Dar es Salaam kwenda Malawi wamekufa papo hapo na wengine zaidi ya 20 kujeruhiwa vibaya katika ajali iliyotokea jioni jana katika eneo la Nyololo wilaya ya Mufindi mkoani Iringa. 
Mmoja kati ya mashuhuda aliyejitambulisha kwa jina la Dkt Matatala alisema kuwa ajali hiyo imetokea JANA mida ya saa 11 jioni wakati basi hilo likitokea Dar es Salaam kwenda
nchini Malawi. 
Alisema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni lori lenye namba za usajili T 104 DZZ ambalo lilikuwa likitokea Makambako kuelekea Iringa,lori lililokuwa likijaribu kulipita lori lenye namba za usajili T 227 AVC na kushindwa kupita na kuishia kugongana uso kwa uso na basi hilo ambalo pia lilikuwa likija kwa mwendo wa kasi. 
Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo wamesema kuwa ajali hiyo imetokea katikati ya mji wa Nyololo ambapo ni jirani kabisa na eneo lenye matuta ya kuzuia magari kwenda kwa mwendo kasi.
 Alisema kuwa hadi majira ya saa 12.45 jioni maiti tano zilikuwa zimetolewa katika basi hilo la Taqwa na kuwa jitihada za wasamaria wema kutoa maiti na majeruhi katika eneo hilo zimeendelea kufanyika. 
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...