Huko Ujerumani, msemaji wa
serikali amesema kuwa anaheshimu kazi kubwa iliyofanywa na Papa huyu
aliyezaliwa katika Jimbo la Bavaria la nchini humo.
Askofu mkuu wa Canterbury amesema amazipokea taarifa za kujiuzulu kwa Papa kwa huzuni mkubwa ingawa anaelewa undani wa hatua yake.
Kiongozi wa Ujeremani, Bi. Angela Merkel amesifu mchango wa Papa wa kupendekeza mjadala baina ya makanisa, waislamu na wayahudi.
Alikumbusha hotuba ya Papa alipozuru bunge la Ujerumani mnamo mwaka 2011.