Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimekubali kusitisha
maandamano yaliyokuwa yafanyike leo kushinikiza kujiuzulu Waziri wa Elimu na
Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa kutokana na matokeo mabaya ya kidato cha
nne ya 2012.
Makubaliano yalifikiwa baada ya kikao cha Mkuu wa Jeshi la Polisi
Tanzania (IGP), Said Mwema na viongozi wa Chadema walioongozwa na Mwenyekiti wa
Chama hicho, Freeman Mbowe kilichofanyika makao makuu ya jeshi hilo jijini Dar
es Salaam.