Language

Sunday, 21 April 2013

WATU 185 WAPOTEZA MAISHA KATIKA MAPIGANO YA VIKUNDI VYA KIISLAMU NIGERIA


Mapigano ya wapiganaji wa kiislamu na vikosi vya usalama nchini Nigeria yameripotiwa kutokea tangu usiku wa Ijumaa na kuendelea kwa muda mrefu ambapo jumla ya watu 185 wanaripotiwa kufariki dunia katika mapigano hayo yaliyotokea Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyotolewa na Serikali ya mji wa Baga na Ofisa Serikali hiyo Bwana Lawan Kole.
Inasemekana kuwa watu wengi zaidi wamefariki dunia ambapo bado juhudi za kutafuta maiti nyingine zinaendelea. Brigedia Jenarali Austin Edokpaye amewaambia maafisa wakuu wa serikali kuwa,wapiganaji walitumia silaha kali na maroketi yenye mabomu mazito kupambana na vikosi vya jeshi.
Aidha bwana Edokpaye aliongeza kuwa,wapiganaji hao walikuwa wakitumia raia kama kinga yao kwa kujibanza karibu na makazi ya watu ambapo walijua vikosi vya jeshi visingeweza kujibu mapigo.

EXCLUSIVE!!! JUSTIN BIEBER NA SELENA GOMEZ WARUDIANA


Iliwahi kutokea mara ya kwanza Justin Bieber alipokuwa backstage katika moja ya matamasha yake, pia Justin na Selena Gomez wamekutwa wakibusiana (kiss) nyuma ya jukwaa katika shoo aliyofanya Justin mwishoni mwa wiki hii huko Norway.

Shuhuda wa tukio hilo amesema kuwa: “walikuwa wameshikana mikono muda wote, wakikumbatiana mara kwa mara na walikiss midomoni."
Kisha akaendelea"Wanaonekana wako penzini tena katika dimbwi zito la mapenzi, kana kwamba hawajawahi kugombana awali. Wanaonekana kabisa wamerudiana pamoja."
Justin na Selena walivunja uhusiano wao mwishoni mwa  mwaka 2012, lakini wote wawili walithibitisha kuwa bado wanawasiliana vizuri.
Kuna baadhi ya watu wao wa karibu waliwahi kusema kuwa  Gomez alikuwa akimtumia Bieber za kumuumiza pamoja na kumpigia simu na kumkumbushia mambo mengi ya kimapenzi waliyoenjoy pamoja kabla ya kutengana
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...