Iliwahi kutokea mara ya kwanza Justin Bieber alipokuwa backstage katika
moja ya matamasha yake, pia Justin na Selena Gomez wamekutwa wakibusiana (kiss)
nyuma ya jukwaa katika shoo aliyofanya Justin mwishoni mwa wiki hii huko Norway.
Shuhuda wa tukio hilo amesema kuwa: “walikuwa wameshikana mikono muda
wote, wakikumbatiana mara kwa mara na walikiss midomoni."
Kisha akaendelea"Wanaonekana wako penzini tena katika dimbwi zito
la mapenzi, kana kwamba hawajawahi kugombana awali. Wanaonekana kabisa
wamerudiana pamoja."
Justin na Selena walivunja uhusiano wao
mwishoni mwa mwaka 2012, lakini wote
wawili walithibitisha kuwa bado wanawasiliana vizuri.
Kuna baadhi ya watu wao wa karibu waliwahi kusema kuwa Gomez alikuwa akimtumia Bieber za kumuumiza
pamoja na kumpigia simu na kumkumbushia mambo mengi ya kimapenzi waliyoenjoy
pamoja kabla ya kutengana
No comments:
Post a Comment