MOJA
ya mambo yaliyoamsha hisia za wakazi wa Mkoa wa Mtwara hadi kushinikiza
kwa vurugu wakitaka gesi isitoke mkoani humo, ni taarifa kuwa nishati
hiyo ingepelekwa wilayani Bagamoyo, nyumbani kwa Rais Jakaya Kikwete.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alisema jana nyumbani kwake mjini Dodoma kuwa, mbali na imani hiyo, amebaini pia kuwa mpasuko ndani ya CCM mkoani Mtwara na harakati za kisiasa ni sababu nyingine iliyochochea mgogoro huo.
Pinda alikuwa akizungumza na waandishi wa
habari kuhusu mgogoro huo ambao ulisababisha vifo vya watu wanne huku
wengine wakijeruhiwa vibaya na uharibifu mkubwa wa mali zikiwamo nyumba
za wabunge kuchomwa moto na namna alivyofanikiwa kuuzima.
Waziri Mkuu alifanya ziara ya siku mbili
mkoani Mtwara, Januari 25 na 26 mwaka huu na kufanikiwa kuzima mgogoro
huo baada ya kufanya mazungumzo na makundi mbalimbali ya wadau wa gesi
mkoani humo.
“Sasa hili nililitolea ufafanuzi kwa kukanusha kuwa siyo kweli kwamba gesi inakwenda Bagamoyo. Lakini pia baada ya kukaa nao nilibaini kuwa hata viongozi wenyewe wa CCM hawako pamoja,” alisema Pinda na kuongeza:

“Pamoja na hayo nikachukua