MOJA
ya mambo yaliyoamsha hisia za wakazi wa Mkoa wa Mtwara hadi kushinikiza
kwa vurugu wakitaka gesi isitoke mkoani humo, ni taarifa kuwa nishati
hiyo ingepelekwa wilayani Bagamoyo, nyumbani kwa Rais Jakaya Kikwete.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alisema jana nyumbani kwake mjini Dodoma kuwa, mbali na imani hiyo, amebaini pia kuwa mpasuko ndani ya CCM mkoani Mtwara na harakati za kisiasa ni sababu nyingine iliyochochea mgogoro huo.
Pinda alikuwa akizungumza na waandishi wa
habari kuhusu mgogoro huo ambao ulisababisha vifo vya watu wanne huku
wengine wakijeruhiwa vibaya na uharibifu mkubwa wa mali zikiwamo nyumba
za wabunge kuchomwa moto na namna alivyofanikiwa kuuzima.
Waziri Mkuu alifanya ziara ya siku mbili
mkoani Mtwara, Januari 25 na 26 mwaka huu na kufanikiwa kuzima mgogoro
huo baada ya kufanya mazungumzo na makundi mbalimbali ya wadau wa gesi
mkoani humo.
“Sasa hili nililitolea ufafanuzi kwa kukanusha kuwa siyo kweli kwamba gesi inakwenda Bagamoyo. Lakini pia baada ya kukaa nao nilibaini kuwa hata viongozi wenyewe wa CCM hawako pamoja,” alisema Pinda na kuongeza:

“Pamoja na hayo nikachukua
maelezo kuhusu matatizo yao mengine na nikawaahidi kwamba nitayafikisha katika mamlaka husika ili waweze kuona namna ya kufanya.”
maelezo kuhusu matatizo yao mengine na nikawaahidi kwamba nitayafikisha katika mamlaka husika ili waweze kuona namna ya kufanya.”
Madai kwamba gesi hiyo inapelekwa Bagamoyo
yalikuwa moja ya ujumbe mkuu uliokuwa umeandikwa kwenye baadhi ya
mabango wakati wa maandamano ya Desemba 27 mwaka jana yaliyofanyika
Mtwara Mjini, yakiratibiwa na baadhi ya vyama vya siasa vya upinzani.
Pinda alisema viongozi wa kisiasa mkoani
Mtwara wakiwamo wabunge, wameonekana kuwa na mpasuko unaosababisha
uchochezi kwa makundi ya watu.
Alipotakiwa kuzungumzia madai hayo ya Waziri
Mkuu, Katibu wa CCM Mkoa wa Mtwara, Alhaji Masoud Mbengula alikiri chama
hicho kumeguka na akataja sababu kuwa ni makundi yaliyotokana na
uchaguzi wa ndani uliofanyika mwaka jana.
“Tusiwe wanafiki, ni kweli kuna makundi ndani ya chama… wabunge hawako pamoja na ndiyo hali iliyotufikisha hapa… suala hili lipo wazi kabisa,” alisema Alhaji Mbengula.Kamati ya Spika hatihati
Akizungumzia Kamati ya Bunge iliyotarajiwa kuundwa na Spika kwenda Mtwara kwa ajili ya kuwasikiliza wananchi wa huko, Pinda alisema hawezi kuingilia mhimili huo wa Dola isipokuwa atatoa taarifa bungeni na kama Spika ataona wabunge wameelewa, basi ataamua lolote.

“Nitakuwa na nafasi ya kuzungumzia jambo hili
ndani ya Bunge na Spika akiona wabunge wamenielewa bila shaka atasitisha
lakini akiona bado inafaa ataamua yeye,” alisema.
Kabla ya kuzungumza na waandishi wa habari
jana, kiongozi huyo alifanya mazungumzo na Mawaziri wanaotoka Mkoa wa
Mtwara ambao ni George Mkuchika (Utawala Bora) na Hawa Ghasia (Tamisemi)
pamoja na wawekezaji wa kutoka China ambayo alisema yalilenga kuwapa
halihalisi ya huko.
No comments:
Post a Comment