MWANAMUZIKI
wa siku nyingi wa muziki wa kizazi kipya, Judith Wambura Mbibo au Lady Jay Dee,
yuko kwenye matayarisho ya albamu yake ya sita, na tayari ameshatengeneza
nyimbo mbili, mmoja akiwa amefanya mwenyewe na wa pili akiwa amemshirikisha
Profesa Jay, wimbo unaoitwa Joto na Hasira.
Jay Dee ambaye pia ni
mmiliki wa mgahawa wa Nyumbani Lounge, ameliambia gazeti hili kwamba ujio wake
wa safari hii utakuwa wenye ubunifu wa hali ya juu, kutokana na kile anachosema
kwamba ana uzoefu zaidi kuliko ilivyo awali na pia anataka kuzikonga nyoyo za
wapenzi wake.
Maendeleo ya
utengenezwaji wa albamu hiyo yanavyoendelea yatakuwa yakionyeshwa katika
kipindi chake cha Diary ya Lady Jay Dee kinachoonyeshwa na kituo cha
Televisheni cha EATV.