SERIKALI imejiwekea lengo la
kutahiri wanaume milioni 2.8 ifikapo mwaka 2015, baada ya kufanikiwa kuwatahiri
287,055 kati ya mwaka 2010 na 2012.
Hayo yamebainishwa katika taarifa
iliyotolewa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, ikifafanua kuwa huduma ya
tohara ya kitabibu kwa wanaume ilianzishwa mwaka 2010.
Imetekelezwa zaidi mikoa ambayo
ilibainika kuwa na kiwango cha juu cha maambukizi ya virusi vya Ukimwi.
“Iligundulika kiwango cha juu cha
maambukizi ya VVU ambako kuna kiwango cha chini cha tohara kwa wanaume.
Mikoa hiyo ni ya Iringa, Njombe, Simiyu, Geita, Katavi, Mbeya, Rukwa,
Tabora, Kagera, Mwanza na Mara,” inaelezwa taarifa hiyo.
Inaelezwa kuwa Serikali
ilifanikiwa kuwafanyia tohara wanaume hao kwa kutumia njia ya kuwaelimisha kwa
kuwaelezea umuhimu wa tohara na hatari inayowakabili kwa kuendelea kuishi bila
kufanyiwa tohara hasa kuambukizwa magonjwa ya zinaa ikiwamo VVU.
Pia, taarifa hiyo inaeleza kuhusu
mpango wa kuzuia maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto kwa mwaka
2005, wajawazito 11,435 ambayo ni asilimia tisa ya wenye maambukizi ya virusi.
Inasema walipatiwa dawa za ARVs
kuzuia maambukizi hayo kwenda kwa mtoto.
Taarifa hiyo inaeleza kuwa,
wizara hiyo inaendelea kutoa kupaumbele maeneo ya kudhibiti magonjwa ya ngono,
utoaji ushauri nasaha na huduma kwa wagonjwa wa nyumbani, elimu na habari, tiba
na matunzo, huduma ya maabara kwa wagonjwa waishio na VVU.
“Hamasa kwa Watanzania imekuwa
ikiongezeka hasa baada ya kampeni iliyoongozwa na Rais (Jakaya Kikwete) mwaka
2007, idadi ya vituo vya upimaji iliongezeka kutoka vituo 521 mwaka 2005 hadi
2,200 mwaka jana,” inasema taarifa hiyo na kuongeza:
“Iidadi ya wananchi waliopatiwa
huduma hiyo nayo imeongezeka kutoka watu 365,189 mwaka 2005 hadi watu
17,008,475 Machi mwaka jana.”
No comments:
Post a Comment