Vichwa Vya Habari
Language
Wednesday, 16 January 2013
MICHEZO: EMMANUEL OKWI AIAGA RASMI SIMBA SC
SHAMBULIAJI wa Simba SC, Mganda
Emmanuel Okwi ameuzwa klabu ya Etoile du Sahel ya Tunisia kwa dola za
Kimarekani 300,000.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe amesema mida hii kwamba,
Okwi amekamilisha vipimo na kila kitu na tayari amesaini mkataba.
“Tunasubiri
kulipwa fedha zetu tu, viongozi watakwenda Tunisia kuchukua fedha za mauzo ya
mchezaji huyo,”alisema Poppe.
Okwi
amekuwa akipiga chenga kuripoti kambini Simba SC na alikuwa hata hapokei simu
za viongozi wa klabu hiyo kila alipopigiwa.
Kufuatia
hatua hiyo, uongozi ulimuengua kwenye programu ya safari ya Oman na sasa
inabainika ametua Sahel.
Baada ya
kumaliza mkataba wake wa awali, Desemba mwaka jana aliongeza mkataba wa miaka
miwili na Simba SC ambao kabla hajaanza kuutumikia, anahamia Sahel.
HABARI: OLE WAKE ATAKAEICHEZEA SERIKALI
Serikali imesema haitavumilia kwa namna yeyote ile vurugu za
kidini, kikanda na ukabila ambazo baadhi yake zilitaka kulitia doa taifa
mwaka jana.
Pia imesisitiza kwamba haitawavumilia wanasiasa wanaotumia rasilimali za taifa kujitafutia umaarufu kwa gharama za kuligawa taifa.
Pia imesisitiza kwamba haitawavumilia wanasiasa wanaotumia rasilimali za taifa kujitafutia umaarufu kwa gharama za kuligawa taifa.
Akizungumza na mabalozi kwa nyakati tofauti
Ikulu, Dar es Salaam; kwanza katika sherehe ya kuukaribisha Mwaka Mpya
iliyofanyika juzi na alipokuwa akiagana na Balozi wa Uingereza nchini,
Dianne Corner jana, Rais Jakaya Kikwete alisema vurugu zilizotaka
kujitokeza mwaka jana zinatosha.
“Serikali haitavumilia vurugu wala ukabila kwa
namna yoyote ile…. Mwaka 2012 vurugu zenye sura ya kidini zilianza
kujitokeza ila sasa nasema kwamba hatutazivumilia kwa namna yeyote ile,
inatosha,” alisema Rais Kikwete.
Akizungumza katika hafla hiyo, Kiongozi wa
Mabalozi ambaye pia ni Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC),
Juma Mpango alisema jumuiya ya mabalozi imefurahishwa na namna ambavyo
Serikali imekuwa ikishughulikia vurugu za kidini ambazo zilitaka
kujitokeza bila kusababisha madhara kwa wananchi.
“Tumeridhishwa na namna ambavyo Serikali
imekuwa inashughulikia mambo yake vizuri. Tunaomba mwendelee
kushughulikia amani ya nchi hii maana ndiyo mhimili wa nchi za Maziwa
Makuu,” alisema Balozi Mpango.
Kuhusu gesi
Rais Kikwete alizungumzia suala la rasilimali za taifa na kusisitiza kuwa pia hatavumilia kuona wanasiasa wakitumia suala la gesi kujitafutia umaarufu.
Wakati Rais Kikwete akitoa kauli hiyo jana,
habari kutoka Mtwara zilidai kuwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini,
George Simbachawene amewekewa magogo barabarani kumzuia asiende kwenye
kijiji kinachozalisha gesi hiyo, huku Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea,
Regina Chonjo akizomewa.
Hata hivyo, polisi walikiri wananchi kuweka
magogo barabarani kwa lengo la kumzuia waziri huyo, lakini ikaeleza kuwa
gari lililozuiwa siyo la Simbachawene.
Akizungumza na Balozi Corner, Rais Kikwete
alikemea tabia ya baadhi ya viongozi wa kisiasa kutumia suala la
rasilimali za taifa, ikiwamo gesi asilia kujitafutia umaarufu wa kisiasa
na kuwapotosha wananchi.
“Ni jambo la hatari na lisilo na tija kwa
wanasiasa kujaribu kuigawa nchi vipandevipande kwa sababu ya kujitafutia
umaarufu kwa kutumia rasilimali za taifa,” alisema Rais Kikwete na
kuongeza:
“Unawezaje kuwa na nchi moja na taifa moja
wakati kila mmoja anadai rasilimali kutoka kwenye eneo moja ibakie na
kunufaisha watu wa eneo hilo tu. Huwezi kuwa na nchi moja na yenye umoja
wakati kuna nchi ya gesi asilia kule Mtwara, kuna nchi ya kahawa kule
Kilimanjaro, kuna nchi ya chai na ndizi kule Bukoba,” alisema Rais
Kikwete na kuongeza:
“Kwa sababu kama gesi asilia inatakiwa kubakia
na kunufaisha watu wa Mtwara tu, basi wenye haki zaidi ya kudai jambo
hili siyo watu wa Mtwara, bali ni watu wa Msimbati ambako ndiko
ilipogunduliwa gesi ambako ni maili 60 kutoka Mtwara, kilomita 200
kutoka Newala.”
Subscribe to:
Posts (Atom)