Washtakiwa wa kesi inayowakabili viongozi wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara
ya Kidini (Jumiki) Zanzibar, wamesomewa mashtaka mapya katika Mahakama Kuu.
Nassib alidai washtakiwa hao wanakabiliwa na madai ya kuharibu mali,
uchochezi, ushawishi na kuham asisha fujo na kula njama ya kufanya kosa.
Mshtakiwa Azan Khalid (48), anakabiliwa na kosa la ziada peke yake
akidaiwa kufanya vitendo vinavyoweza kusababisha uvunjifu wa amani.
Alidai makosa yote hayo yalifanyika kati ya Oktoba 17, 18 na 19 maeneo
tofauti na washtakiwa wote walikana madai hayo.
Licha ya Azan, washtakiwa wengine ni Masheikh Farid Hadi (41), Mselem
Ali Mselem (52), Mussa Juma Mussa (47), Suleiman Juma Suleiman (66), Khamis Ali
Suleiman (59) na Hassan Bakar Suleiman (39).
Nassib alidai kuwa upelelezi umekamilika, lakini aliomba Mahakama
kufanya subira ya kutoa uamuzi wowote vile upande wao umekata rufani Mahakama
ya Rufaa na unaweza ukaathiri uamuzi wa Mahakama hiyo.
Mawakili wa watetezi ukiongozwa na Taufik Salum uliomba Mahakama hiyo,
kuwapatia dhamana washtakiwa hao kwa vile wako rumande muda mrefu.
Jaji Mahmoud alisema atapitia kwa undani maombi ya pande zote mbili,
kwa vile ni mgeni katika kesi hiyo na atatoa uamuzi.
Aliahirisha kesi hiyo hadi kesho.
No comments:
Post a Comment