TIMU ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' imefika salama Addis Ababa
tayari kwa mechi ya kirafiki dhidi ya wenyeji Ethiopia. Mechi hiyo
itachezwa kesho (Januari 11) katika Uwanja wa Addis Ababa kuanzia saa
11.30 jioni. Stars imefikia katika hoteli ya Hilton na itafanya mazoezi
leo jioni kwenye Uwanja wa Addis Ababa kwa saa moja kuanzia saa 11.30
jioni.
Imetolewa na:
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania