Mwili wa mareheu rais Hugo Chavez wa Venezuela, umelazwa katika kituo cha
mafunzo ya jeshi katika mji mkuu Caracas
Taarifa zinazohusiana
Watu wengi waliangua kilio huku wakichukua picha za kiongozi wao
aliyefariki dunia .
Mama yake na watoto wake walikusanyika mbele ya jeneza kutoa heshma zao
.
Makamu wa rais Nicolas Maduro anaongoza shughuli hiyo.
Mwili wa rais Chavez umepelekwa katika chuo cha kitaifa cha mafunzo ya
kijeshi ambapo utazikwa kesho Ijumaa.
Maelfu ya watu awali walikwenda barabarani mjini Caracas kutoa heshima
zao za mwisho kwa Chavez wakifuatana na gari lililokuwa limebeba jeneza lake
kuelekea katika chuo cha mafuzno ya jeshi.
Mazishi ya kitaifa ya Chavez yatafanyika Ijumaa.
Mkuu wa ulinzi wa Rais alinukuliwa akisema kuwa alikuwa na bwana Chavez
alipofariki.
Generali Jose Ornella, alisema kuwa Chavez alifariki kutokana na
mshtuko wa moyo na katika siku zake za mwisho kabla ya kifo cha ealisema
angependa kuendelea kuishi.
Jeneza lake lililokuwa limefunikwa bendera ya nchi hiyo uliwekwa katika
ukumbi ambao ni kumbukumbu ya waliopigania uhuru wa watu wa Amerika ya Kusini
Maelfu ya watu walipanga foleni kutoa heshima zao za mwisho kwa
marehemu Chavez, wakiwemo maafisa wa serikali na viongozi wa Amerika ya
Kusini,kama Rais wa Bolivia Evo Morales na Rais wa Argentina Cristina Fernandez
de Kirchner.
No comments:
Post a Comment