Papa Francis wa kwanza,kutokana na umri wake mkubwa na mwelekeo wake wa kihafidhina,haonyeshi kama atafanikiwa kulifanyia mageuzi kanisa katoliki,yanayoambatana na wakati tulio nao.
Wahenga wanasema mkamia maji hayanywi" hapa ikimaanisha anaeingia
katika mkutano wa siri akipewa nafasi nzuri ya kuchaguliwa kuwa Papa,anatoka mkutanoni
kama kadinali tu.Kwasababu hakuna yeyote kati ya waliopigiwa upatu
wangechaguliwa
kuwa kiongozi wa kanisa katoliki
ulimwenguni,aliyechaguliwa-badala yake makadinali wamemchagua mchamungu ambae
amejipatia umashuhuri kutokana na kutopenda makubwa pamoja na juhudi zake za
kuwapigania wasiojiweza .Kardinali wa ki-Argentina Jorge Mario
Bergoglio,aliyechagua jina la Francis wa kwanza,ni Papa wa kwanza ambae hatokei
Ulaya.Nchini mwake,amedhihirisha anapenda sana kuwa karibu na watu na anazijua
kikamilifu dhiki na shida za watu maskini.Hilo pekee linawapa matumaini mema
wakatoliki wanaoishi katika maene ya mabanda,madongo poromoka na kambi za
wakimbizi katika kila pembe ya dunia.Katika eneo la Latin Amerika matumaini
yalikuwa makubwa ya kumpata Papa anaetambua hali zao za maisha.
Hata mrithi huyu wa sasa wa mjumbe wa Mungu Petrus ni mhafidhina- jambo
ambalo si la kustaajabisha - watangulizi wake wote wawili na kwa kipindi cha
miaka 35 iliyopita walikuwa wakiwachagua maaskofu wakuu wa kihafidhina kuwa
makadinali na kwa namna hivyo kuwapatia fursa ya kumchagua Papa.Francis wa
kwanza kwa hivyo hawezi kuwa mwanamageuzi ambae wakosoaji wa kanisa
wangependelea achaguliwe.Muumini huyo wa madhehebu ya Jesuit anaitumia kila
fursa inayojitokeza kukosoa kwa maneno makali ukosefu wa usawa katika
jamii-hata hivyo yeye mwenyewe anatajikana kuwa karibu zaidi na jumuia ya
wahafidhina sugu wa kikatoliki:"Comunione e Liberazione".Theolojia ya
ukombozi" haikuwa shetani wake.Sasa jee Papa kama huyu anaweza kuyawekea
suala la kuuliza mafunzo ya dini ya kikatliki?
Na jee watu wanaweza kumpongeza Papa huyu?
Majukumu na matatizo yanayomsubiri mchamungu huyo mwenye umri wa miaka
76 ni makubwa kupita kiasi.Kwanza kabisa Papa Francis wa kwanza anabidi
arejeshe imani ya waumini.Kashfa ya kuingiliwa kimwili watoto na vijana na
wachamungu wa kikatoliki kimechafua sana hadhi ya kanisa na hasa katika nchi za
magharibi ambako umati wa waumini wanalipa kisogo kanisa.
Francis wa kwanza analazimika kuanzisha mageuzi yanayohitajika ya
kanisa na ambayo yalikuwa yaanze tangu zamani.Kuna suala la kuwepo tabaka mbili
za jamii kati ya maaskofu na watu wanaojitolea kulitumikia kanisa,sura hiyo
inabidi ibadilishwe na kuimarisha nafasi ya waumini wanaolitumikia kanisa kwa
kujitolea.Wakinamama, ambao ndio wanaotekeleza sehemu kubwa ya shughuli za
kanisa wanastahiki kuzingatiwa.Mjadala wa uwazi kwa wale wanaounga mkono na
wengine wanaopnga utawa unabidi uendelezwe.Kitheolojia watu wanasubiri pia
kuona vipi litashughulikiwa suala la watu walioachana na kuowa au kuolewa na
mtu mwengine.Uhusiano pamja na makanisa ambayo si ya kikatoliki na hasa yale ya
wapenda mageuzi nao ia unahitaji kuchunguzwa.Mdahalo kati ya waumini wa dini
tofauti unabidi uendelezwe na mengi menginyo.
Si wa kumezewa mate
Lakini hata Vatikan kwenyewe kuna yanayobidi kushughulikiwa.Kashfa ya
kuibiwa hati za siri za Papa,visa vya kichini chini vya hadaa na kutiliana
fitna yote hayo yamezidisha dhana kwamba Papa Benedkt wa 16 alishindwa
kuidhibiti hali ya mambo.
Hasha,hakuna anaeumezea mate wadhifa wa kiongozi wa wakatoliki bilioni
moja nukta mbili.Pekee umri wake mkubwa unamfanya mtu ashuku kama kweli yeye
ndie anaefaa.Yadhihirika zaidi kana kwamba makadinali wamemchagua Papa wa
kipindi cha mpito na wala hawajachagua mkonndo mpya.Pengine mkutano wa
siri,kutokana na hali inayolikabili kanisa katoliki imeipoteza fursa
iliyojitokeza.Lakini si kuna usemi usemao imani huzusha miujiza.
No comments:
Post a Comment