Kadinali Bergoglio anakuwa mtu wa kwanza kutoka Amerika kusini
kuchaguliwa kuwa Papa.
Awali moshi mweupe ulishuhudiwa ukifuka kutoka bomba la kutolea moshi
katika kanisa la Sistine Chapel na kufuatiwa na kengele kupigwa. Hii ilikuwa ni
ishara kwa walimwengu kuwa makadinali ambao walianza mchakato wa kumchagua Papa
mpya hatimae walikuwa wamefaulu katika kazi yao.
Kadinali Bergoglio anachukuwa mahali pa Papa Benedict XVI, ambaye
alijiuzulu mwezi uliopita akisema hana nguvu na uwezo wa kuendelea kuliongoza
Kanisa Katoliki.
Makadinali 115 wamekuwa faraghani tangu siku ya Jumanne alasiri na
wakaanza mchakato wao kwa kupiga kura mara nne kwa siku.
Ilikuwa inahitajika kuwa angalau Makadinali 77 yaani theluthi-mbili
wangeliweza kumpigia kura mmoja wao ili aweze kutangazwa kuwa Papa mpya.
Na kabla ya mchakato huo kuanza kulikuwa hakuna dalili za kuonyesha
nani angelichaguliwa.
Maelfu ya watu kutoka sehemu mbali mbali duniani walikwa wamekusanyika
katika ukumbi wa Kanisa la St Peter tangu siku ya Jumanne.
Muda mfupi kabla ya Kadinali Bergoglio kujitokeza , maelfu ya watu
walionekana wakikimbia kuelekea ukumbi wa St Peters ili kuweza kumshuhudia Papa
mpya akitangazwa
No comments:
Post a Comment