Bunge la uteuzi nchini China limemteua kiongozi wa Chama cha Kikomunisti,
Xi Jinping, kuwa rais hatua inayomuweka kwenye kilele cha madaraka ya taifa
hilo linalokuwa kwa kasi kubwa ya kiuchumi duniani.
Xi Jinping aliinama kwa heshima juu ya jukwaa kuu katika Ukumbi Mkuu wa
Watu wa China, kama linavyoitwa jengo la bunge la nchi hiyo, huku wajumbe
wakimpigia makofi ya kumpongeza katika tukio hilo lililorushwa moja kwa moja na
televisheni ya taifa.
Kati ya kura 2,961 zilizohisabiwa, ni kura moja tu iliyomkataa, huku
wajumbe watatu wakiripotiwa kutokuhudhuria mkutano huo maalum wa uteuzi. Kwa
hivyo, akiwa mgombea pekee wa nafasi hiyo, Xi amepitishwa kwa asilimia 99.7 ya
kura.
Tayari Xi alishachukua nafasi ya ukuu wa chama cha Kikomunsti kutoka
kwa Hu hapo mwezi Novemba, na kabla ya kura ya leo kupigwa, mikutano ya awali
ya viongozi wa kisiasa wa baraza hilo ilishalipitisha na kulipendekeza jina
lake.
No comments:
Post a Comment