Wafuasi wa Chadema, wameibua tafrani ya aina yake wakati wa mazishi ya
aliyekuwa Mjumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), marehemu
Benson Mollel baada ya kung’oa bendera za chama hicho na kuamsha hasira za
waombolezaji wafuasi wa chama tawala.
Mollel alikutwa amefariki mwanzoni mwa wiki, katika Hoteli ya Lush Garden
Business, Mtaa wa Jacaranda Arusha huku mwili wake ukiwa mtupu.Tukio hilo
lilitokea usiku wa kuamkia jana na baadhi ya makada wa CCM walionekana
wakiwasaka wafuasi hao wa Chadema.