Wakenya watakwenda kupiga kura hapo Machi 4 kumchagua kiongozi
atakayeiongoza nchi hiyo. Wagombea wa kiti cha urais watafanya mjadala
wa
Vichwa Vya Habari
Language
Monday, 25 February 2013
MICHEZO:NIYONZIMA"TUTALIPA KISASI KWA KAGERA SUGAR
KIUNGO wa Yanga, Haruna Hakizimana Fadhil Niyonzima, amesema kwamba watalipa kisasi cha kufungwa 1-0 na Kagera Sugar wakati watakaporudiana na timu hiyo kesho, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Akizungumza na BIN ZUBEIRY jana, Niyonzima alisema kwamba wamepania kushinda mechi zote zilizobaki za Ligi Kuu ili kuchukua ubingwa kwa heshima kubwa.Amesema kwanza lazima walipe kisasi cha kufungwa na Kagera katika mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu, mwaka jana Uwanja wa Kaitaba, Bukoba.
“Kagera walitufunga Bukoba, na sisi lazima tuwafunge hapa Jumatano. Lakini kikubwa ni kampeni yetu ya kushinda kila mechi ili tuchukue ubingwa kwa heshima kubwa,”alisema.
Nahodha huyo wa timu ya taifa ya Rwanda, alisema
HABARI MUHIMU: ANALOJIA KUZIMWA MWANZA FEBRUARI 28
MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imesema inatarajia kuzima matangazo ya mfumo wa analojia mkoani hapa Februari 28, mwaka huu, hivyo kuwataka wananchi kuchangamkia fursa ya kujiunga na mfumo mpya wa utangazaji wa dijitali.
Mkurugenzi wa Utangazaji wa TCRA, Habbi Gunze, alibainisha hayo jana alipozungumza na waandishi wa habari mjini hapa.
Alisema matangazo rasmi ya mfumo wa dijitali mkoani hapa Machi mosi mwaka huu, na kwamba TCRA ipo kwenye mchakamchaka wa kutekeleza mipango yake ya makubaliano na nchi nyingine za Afrika Mashariki katika suala zima la kujiunga na mfumo wa dijitali.
Mkurugenzi wa Utangazaji wa TCRA, Habbi Gunze, alibainisha hayo jana alipozungumza na waandishi wa habari mjini hapa.
Alisema matangazo rasmi ya mfumo wa dijitali mkoani hapa Machi mosi mwaka huu, na kwamba TCRA ipo kwenye mchakamchaka wa kutekeleza mipango yake ya makubaliano na nchi nyingine za Afrika Mashariki katika suala zima la kujiunga na mfumo wa dijitali.
HABARI MUHIMU: PADRI WA UINGEREZA ALIYEJIUZULU KISA KASHFA YA NGONO HUYU HAPA
Mmoja wa mapadre waandamizi wa kanisa
katoliki nchini Uingereza amejiuzulu wadhifa wake kufuatia shutma za
kwamba alikwenda kinyume na matakwa ya kipadre mapema miaka ya
themanini.
Kardinal Keith O'Brien ameachia madaraka kama
kiongozi mkuu wa kanisa katoliki nchini Scotland na hatarajii kusafiri
kwenda Vatican baadaye mwaka huu kumchagua Papa ajaye baada ya baba
Mtakatifu Benedict wa 16 kijuzuru.
BBC imeelezwa kuwa kiongozi
huyo,ameshutumiwa na mapadre watatu wa kanisa hilo na hatua hiyo ya
kujiuzulu ni tukio kubwa katika mwenendo wa kanisa katoliki ikizingatiwa
kuwa Kanisa hilo limekuwa kwenye shutma za ulaji rushwa na matatizo ya
kiongozi kwa siku za hivi karibuni.
HABARI MUHIMU: HUU NDIO MTANDAO WA UJAMBAZI MBEYA DAR ES SALAAM, IRINGA NA MOROGORO
POLISI mkoani Mbeya kwa kushirikiana na polisi mkoani Iringa wamegundua mtandao wa majambazi Sugu ambao umekuwa ukihusika na matukio ya mauaji na unyang’aji wa kutumia silaha.
Kamanda wa polisi mkoani hapa Diwan Athumani amesem leo(Feb 25) kuwa watu 13 wakiwemo askari wawili wanashikiliwa huku wengine 16 wakiendelea kufanyiwa uchunguzi na jeshi hilo. Kamanda Athumani aliwataja askari waliokamatwa kuhusika na mtandao huo kuwa ni MT 85393 Samwel Balumwina(31) wa kikosi cha 844 KJ cha Jeshi la kujenga Taifa(JKT) Mbeya na polisi G 9101 PC Samwel Kigunye(27) wa kikosi cha kutuliza ghasia(FFU) Mbeya. Alisema askari hao wamekuwa wakihusika na mtandao wa ujambazi kwa kuazimisha sare za polisi na jeshi la wananchi(JWTZ) kwa wenzao wanaokwenda katika matukio ya uvamizi na kusisitiza kuwa
Subscribe to:
Posts (Atom)