POLISI mkoani Dar es Salaam wametangaza kuwafuatilia, kuwasaka na kuwachukulia hatua wote waliotuma ujumbe wa matusi ama kupiga simu ya vitisho kwa Spika wa Bunge, Anne Makinda.
Viongozi wa Chadema walifanya mkutano wao
mwishoni mwa wiki kwenye Viwanja vya Mwembe Yanga, Temeke, jijini Dar es
Salaam na kutoa namba za Spika wa Bunge ili mashabiki wamshinikize
ajiuzulu.
Pia viongozi hao walitoa namba za simu za Naibu Spika, Job Ndugai ili naye ashinikizwe ang’oke katika nafasi yake kwa madai ya kukandamiza upinzani bungeni.
Pia viongozi hao walitoa namba za simu za Naibu Spika, Job Ndugai ili naye ashinikizwe ang’oke katika nafasi yake kwa madai ya kukandamiza upinzani bungeni.
Chadema walidai kuwa Makinda na Ndugai