Language

Friday, 8 March 2013

BURUDANI: KANYE WEST AGOMA NAFASI YA 7 ALIYOPEWA NA MTV KATIKA MTV HOTTEST MCs


Manager na C.E.O wa G.O.O.D MUSIC Rapper Kanye West,Amezungumza
kwenye Show ya Angie Martinez wa HOT 97 na Kuzungumza na DJ Enuff
Kuhusu Alivyojisikia yeye kukamata nafasi ya 7 kwenye orodha ya
Mtv Hottest MCs.....
Yeezy Amemueleza Enuff kuwa Anadhani Rapper Lil Wayne ndo MCs Mkali zaidi
kwenye game....amefurahi pia kuona Big Sean kuingia kweneye Top 5
but Yeye kama yeye alipaswa kuwepo kwenye Top 5 hiyo na sio namba 7.
Baba Huyo Mtarajiwa wa Kim Kardashian Ameendelea kusema; Hakuna
verse kali Mwaka Huu aliyoimba kwenye Remix ya wimbo wa Rihana
wa Diamonds...!
Pia Amemkumbusha DJ Enuff kuwa ni yeye ndie aliempa SWAY (Mwandaaji
wa MTV Hottest MCs) Kipindi cha kwanza cha Tv na Kisha akakata
Simu....!

HABARI MUHIMU: BABA MKWE WA OSAMA BIN LADEN KUFIKISHWA MAHAKAMANI MAREKANI


Mkwe wa kiume wa Osama bin Laden anatarajiwa kufika mbele ya mahakama moja mjini New York Marekani leo Ijumaa kwa mashtaka ya kupanga njama ya kuwauwa Wamarekani.

Sulemain Abu Ghaith ambaye ni mwanamgambo aliyeonekana katika mikanda ya video akiwakilisha mtandao wa kigaidi wa Al Qaeda baada ya mashambulio Septemba mwaka 2001,alikamatwa nchini Uturuki wiki iliyopita na kusafirishwa hadi Marekani kushitakiwa.

HABARI ZA UCHAGUZI MKUU KENYA: SHAMRASHAMRA ZIMEANZA BAADA YA UHURU KENYATTA KUTANGAZWA MSHINDI KATIKA MATOKEO YA AWALI

Uhuru Kenyatta na William Rutto wakifurahia matokeo ya awali


Wafuasi wa Uhuru Kenyatta wakifurahia matokeo ya awali yaliyomtangaza Kenyatta kuwa mshindi wa kiti cha urais


MICHEZO: SIMBA YAMKABIDHI MALKIA WA NYUKI MADARAKA

Baada ya siku moja kupita kufuatia viongozi wawili wa kamati ya utendaji ya Simba kutangaza kujiuzulu, mwenyekiti wa baraza la wadhamini la klabu ya Simba mzee Joseph Itangile maarufu kama mzee Kinesi hii leo ametangaza mabadiliko ya dharura ya  uongozi wa klabu ya klabu hiyo.

Katika mabadiliko hayo mzee Kinesi amesema kuanzia hii jana nafasi iliyokuwa ikishikiliwa na Hans Poppe aliyekuwa mwenyekiti wa kamati ya usajili ya klabu hiyo sasa itakuwa ikishikiliwa na Bi Rahma Al Harouz( malkia wa nyuki) huku nafasi ya makamu mwenyekiti wa klabu hiyo iliyokuwa ikishikiliwa na Geoffrey Nyange Kaburu sasa itakuwa ikikaimiwa na yeye mwenyewe.
Mabadiko hayo yamefuatia kikao cha dharura cha wajumbe wa kamati ya utendaji ya Simba kilicho fanyika jana usiku bila ya kuwepo mwenyekiti Alhaji Ismail Aden Rage ambaye yuko nchini India akifanyiwa matibabu ambaye hata hivyo baada ya mawasiliano kufanyika alikubali na kubariki mabadiliko hayo.
Mzee Kinesi amesema kwamba kwasasa klabu ya Simba bado ina umoja na katika kipindi hiki wameunda kamati ya ushindi ambayo itakuwa chini ya Malkia wa nyuki na kwamba ni wakati wa kuondoa mipasuko ndani ya klabu hiyo.
Jioni hii uongozi wa klabu ya Simba umetembelea tawi la mpira pesa kwa lengo la kuvunja mpasuko ndani ya klabu hiyo na kujenga umoja.

HABARI MUHIMU: HIZI NDIO HABARI 10 KUBWA DUNIANI ZA MACHI 9 KWA UFUPI

Kenya count 'gives Kenyatta victory' Saturday, March 09, 2013 07:18:15 AM
Provisional results give Kenya's Deputy Prime Minister Uhuru Kenyatta a narrow victory in the presidential election, but the official result is due later.
Venezuela swears in acting president Saturday, March 09, 2013 04:59:10 AM
Venezuela's former vice-president Nicolas Maduro is sworn in as acting president hours after the state funeral of Hugo Chavez.

UTABIRI WA HALI YA HEWA KWA MIJI MIKUU A.MASHARIKI LEO MACHI 9


MICHEZO: MATOKEO YA MECHI KUBWA ZA MACHI 8 NDIO HAYA


HABARI ZA UCHAGUZI MKUU KENYA: UHURU KENYATTA KUWA RAIS MPYA KENYA


Matokeo ya mapema ya uchaguzi wa urais nchini Kenya yanaonyesha Uhuru Kenyatta ameshinda na kuepuka raundi ya pili ya uchaguzi. Takwimu kutoka tume ya uchaguzi zinasema Kenyatta ameshinda asilimia hamsini nukta tatu za kura zote zilizopigwa.

Lakini tume ya uchaguzi itakagua hesabu hiyo kabla ya kutangaza matokeo baadaye leo jumamosi, siku tano baada yawakenya kupiga kura.

HABARI MUHIMU: MBUNGE ROSE KAMILI ANATAFUTWA NA POLISI


Polisi Mkoa wa Manyara inamsaka Mbunge wa Viti wa Mkoa wa Manyara(Chadema), Rose Kamili pamoja na watu wengine wanne kwa tuhuma za kufunga ofisi ya kijiji cha Basotu kwa zaidi ya wiki moja sasa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Akili Mpwapwa alisema jana kuwa wanamsaka mbunge huyo,pamoja na wenzake ili watowe maelezo kuhusiana na tukio hilo kabla ya kufikishwa mahakamana.
Mbunge Kamili alipoulizwa jana kuhusiana na kusakwa huko, alikiri kupata taarifa lakini akasema,kama polisi wanamuhitaji wamfuate nyumbani  kwani wanapajua.

HABARI MUHIMU: DAWA ZA KUTULIZA MAUMIVU ZINAMADHARA MAKUBWA KIAFYA, SOMA HAPA

Dawa maarufu za maumivu zilizozagaa katika maduka ya dawa nchini zinatajwa kuchangia ugonjwa wa kiharusi, moyo, vidonda vya tumbo na vifo vya ghafla, imebainika.

Imeelezwa kuwa watu wanaotumia dawa za kutuliza maumivu za Ibuprofen, Diclofenac na Diclopar mara kwa mara wapo katika hatari ya kupata maradhi ya moyo na kiharusi kwa asilimia 40 na hufa vifo vya ghafla.

BURUDANI: KAMA WEWE NI MDAU WA MUZIKI TZ, HII INAKUHUSU MOJA KWA MOJA


BURUDANI: HIZI NDIO NYIMBO 10 AMBAZO WATU WAMEZITWEET ZAIDI WIKI HII


BURUDANI: LIST YA NYIMBO KUMI AMBAZO ZIMEKUWA DOWNLOADED ZAIDI WIKI HII HIZI HAPA


HABARI MUHIMU:MTU ALIYE BADILIKA KUWA ALBINO RUNGWE...STORY KAMILI IKO HAPA


MTU mmoja mkazi wa Kijiji cha Igogwe kata ya Bagamoyo wilayani Rungwe mkoani hapa amebadirika ghafra na kuwa mlemavu wa ngozi (Arbino).

Akisimulia maajabu hayo mtu huyo  Neema  Masebo (26) alisema kuwa alipatwa na mkasa huo alipokwenda kijijini kwao kuwasalimia wazazi wake akitokea nyumbani kwake jijini Mbeya.
Neema alisema kuwa Mama yake mzazi Tumaini Mlawa alipoona hali hiyo alimkimbiza katika hospital ya Wilaya ya Rungwe Makandana kwa ajili ya matibabu ambapo alilazwa siku 7 lakini hali yake ikaanza kubadirika kuwa mbaya huku ngozi yake ikianza kuchubuka taratibu hadi alipobadilika na kuwa mlemavu wa ngozi yaani (Albino).

BURUDANI: HII NDIO LIST YA NYIMBO ZILIZOPATA LIKES NYINGI ZAIDI KATIKA FACEBOOK NA TWITTER WIKI HII


MICHEZO: KAMA HUKUZIJUA, BASI HIZI NDIO MECHI KUBWA ZILIZOKUWA ZINASUBILIWA LEO KATIKA VIWANJA MBALI MBALI DUNIANI


BURUDANI: BEEF YA CHRIS BROWN NA DRAKE BADO MOTO

Chris’ beef with Drake seemed to be far from over as the ‘Turn Up The Music’ artist blasted Drake in front of a packed Hollywood night club on Mar. 6, but a source tells Hollywood.com EXCLUSIVELY that it’s not as serious as it may seem! Read on for the explosive details.

Chris Brown unleashed serious venom towards Drake on Mar. 6 at the Emerson Theatre in Hollywood. The singer reportedly made the DJ, who was playing Drake’s song “Started From The Bottom,” stop the music so he could address the crowd and say “f**k Drake.”
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...