Baada ya siku moja kupita kufuatia viongozi wawili wa kamati ya utendaji
ya Simba kutangaza kujiuzulu, mwenyekiti wa baraza la wadhamini la klabu ya
Simba mzee Joseph Itangile maarufu kama mzee Kinesi hii leo ametangaza
mabadiliko ya dharura ya uongozi wa klabu ya klabu hiyo.
Katika mabadiliko hayo mzee Kinesi amesema kuanzia hii jana nafasi
iliyokuwa ikishikiliwa na Hans Poppe aliyekuwa mwenyekiti wa kamati ya usajili
ya klabu hiyo sasa itakuwa ikishikiliwa na Bi Rahma Al Harouz( malkia wa nyuki)
huku nafasi ya makamu mwenyekiti wa klabu hiyo iliyokuwa ikishikiliwa na
Geoffrey Nyange Kaburu sasa itakuwa ikikaimiwa na yeye mwenyewe.
Mabadiko hayo yamefuatia kikao cha dharura cha wajumbe wa kamati ya
utendaji ya Simba kilicho fanyika jana usiku bila ya kuwepo mwenyekiti Alhaji
Ismail Aden Rage ambaye yuko nchini India akifanyiwa matibabu ambaye hata hivyo
baada ya mawasiliano kufanyika alikubali na kubariki mabadiliko hayo.
Mzee Kinesi amesema kwamba kwasasa klabu ya Simba bado ina umoja na
katika kipindi hiki wameunda kamati ya ushindi ambayo itakuwa chini ya Malkia
wa nyuki na kwamba ni wakati wa kuondoa mipasuko ndani ya klabu hiyo.
Jioni hii uongozi wa klabu ya Simba umetembelea tawi la mpira pesa kwa
lengo la kuvunja mpasuko ndani ya klabu hiyo na kujenga umoja.
No comments:
Post a Comment