Matokeo ya mapema ya uchaguzi wa urais nchini Kenya yanaonyesha Uhuru
Kenyatta ameshinda na kuepuka raundi ya pili ya uchaguzi. Takwimu kutoka tume
ya uchaguzi zinasema Kenyatta ameshinda asilimia hamsini nukta tatu za kura
zote zilizopigwa.
Lakini tume ya uchaguzi itakagua hesabu hiyo kabla ya kutangaza matokeo
baadaye leo jumamosi, siku tano baada yawakenya kupiga kura.
Uhuru amepata
asilimia hamsini nukta sufuri tatu na kuzuia kutokea kwa duru ya pili ya
uchaguzi.
Matokeo yaliyotolewa na tume ya uchaguzi yanaonyesha kuwa Uhuru alipata
kura 6,173,433 huku mpinzani wake Raila Odinga akipata 5,340,546
Kenyatta anakabiliwa na mashtaka katika mahakama ya kimataifa ya ICC
kuhusiana na ghasia za baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2007.
Waandishi wa BBC wanasema iwapo Kenyatta atakabidhiwa ushindi katika
raundi ya kwanza, mpinzani wake waziri Mkuu Raila Odinga atakwenda mahakamani
kupinga matokeo hayo.
Tume ya uchaguzi itatangaza matokeo rasmi ya mshindi baadaye leo
Tume hiyo pia itatangaza mshindi wa uchaguzi huo na vile vile kama
mshindi huyo ametimiza masharti ya kikatiba ya kutangazwa kuwa rais wa nne wa
Kenya.
Kamishna Yusuf Nzibo alitoa taarifa hiyo kwa niaba ya Mwenyekiti wa
Tume Isaack Hassan.
Vile vile mgombea huyo pia lazima awe ameshinda asilimia 25% katika
nusu ya County zote 47 nchini kenya.
Awali Waziri Mkuu Raila Odinga alikuwa amewaalika waandishi wa habari
nyumbani kwake kwa mkutano maalum ili azungumzie maswala ya matokeo ya urais
lakini baadaye mkutano huo uliakhirishwa hadi siku ya Jumamosi , baada ya tume
ya uchaguzi kutoa tangazo lake la mwisho.
No comments:
Post a Comment