Polisi Mkoa wa Manyara inamsaka Mbunge wa Viti wa Mkoa wa Manyara(Chadema),
Rose Kamili pamoja na watu wengine wanne kwa tuhuma za kufunga ofisi ya kijiji
cha Basotu kwa zaidi ya wiki moja sasa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Akili Mpwapwa alisema jana kuwa
wanamsaka mbunge huyo,pamoja na wenzake ili watowe maelezo kuhusiana na tukio
hilo kabla ya kufikishwa mahakamana.
Mbunge Kamili alipoulizwa jana kuhusiana na kusakwa huko, alikiri
kupata taarifa lakini akasema,kama polisi wanamuhitaji wamfuate nyumbani
kwani wanapajua.
Hata hivyo, alisema uamuzi wa kufungwa ofisi hiyo, yalitolewa kwenye
mkutano wa mkuu wa kijiji,kutokana na kupinga unyanyasaji wa viongozi wa
kijiji, kutosoma mapato na matumizi tangu mwaka 2007 na pia kuwataka wafike
Basotu viongozi wa wilaya.
Wananchi 365 walioshiriki mkutano mkuu huo wa kijiji, licha ya kufunga
ofisi hiyo pia walichagua vijana waliopitia mafunzo ya mgambo kulinda ofisi
hizo hadi muafaka utakapopatikana.
No comments:
Post a Comment