MAKAMU wa Rais Dkt. Mohamed Gharib Bilal, leo anafungua mkutano wa
kimataifa wa Afya ya Mama ambao utahusisha washiriki kutoka zaidi ya
nchi 68 wakiwemo wanasiasa.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Arusha jana, Mkurugenzi wa Asasi ya Management and Development for Health (MDH), Dkt. Chalamila Guerino, alisema mkutano huo utakuwa na manufaa kwa afya ya wanawake wajawazito ambao kila siku wanapoteza maisha wakati wa kujifungua.Alisema
mkutano huo utakuwa wa siku tatu, utajadili changamoto mbalimbali
wanazopata wajawazito kwenye uzazi na utafungwa Januari 17 mwaka huu na
Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete.“Mkutanio huu utakuwa na
washiriki wasiopungua 700, wakiwemo wanasiasa ambao watapewa mbinu
mbalimbali zitakazowasaidia kujua masuala ya afya ya mama ili kupunguza
vifo vinavyotokea.“Wanasiasa watapewa mbinu na elimu ya
kuzungumza na wananchi ili jamii iweze kuepukana na vifo vinavyochangia
umaskini nchini,” alisema Dkt. Guerino.Akizungumzia vifo vya
wajawazito hasa wakati wa kujifungua, alisema Tanzania bado inakabiliwa
na changamoto hasa maeneo ya mijini ambayo vifo ni vingi.“Takwimu
za kidunia nazo zinaonesha kuwa, asilimia kubwa ya wanawake wanapoteza
maisha hasa wakati wa kujifungua, nchini Tanzania wanawake 454, kati ya
100,000 hufariki dunia wakati wa uzazi huku.“Kwa nchi
zinaendelea duniani, wanawake 300,000 hufariki dunia hivyo tunapaswa
kupambana na hali hii haraka kwa kuhusisha makundi mbalimbali pamoja na
wanasiasa,” alisema.Alisema kwa upande wa mijini nchini,
changamoto bado ni nyingi ambapo ili vifo hivyo viweze kuwa historia,
lazima tuwe na umoja ambao ni thabiti ili kuokoa maisha ya wanawake.
Aliongeza
kuwa, mkutano huo pia utajadili upatikanaji wa vitendea kazi ili
kuboresha huduma ya afya kwa wajawazito na upimaji ubora ambapo kupitia
mada hizo, Tanzania itaweza kuepusha vifo vingi vya wanawake wajawazito.