Kama unakumbuka msanii Jackline Wolper alimpatia sh mil 16 Sajuki kwa ajili ya matibabu nchini India,
sasa yameanza kuibuka mengine ambapo inadaiwa kuwa kiasi hicho cha
fedha alichukua kwa mtu na mwenye nazo ameshindwa kuvumilia ameamua
kuanza kumdai ili azirudishe tofauti na makubaliano yalivyokuwa.
Inadaiwa kuwa habari hizo zilianza kuzuka tangu siku ambayo Sajuki
amefariki, huku mwenye fedha hizo akidai kuwa alitoa fedha hizo kwa
makubaliano kwamba atarudishiwa mapema lakini hadi muda waliopangwa
umepita haoni dalili zozote za kupewa fedha zake.
Chanzo kimoja cha kuaminika kilizungumza na mwandishi wetu kutoa story ilivyo, ambapo kilidai kuwa ishu hiyo imeanza kujitokeza
upya siku ya msiba na wenyewe walitaka kulipana kimya kimya lakini
baada ya maneno kuwa makubwa wamepanga kulipana muda wowote sasa.
Hata hivyo chanzo hicho kilisema kuwa Wolper hakutakiwa kutoa kiasi
chote cha pesa kwa Sajuki lakini alifanya hivyo ili kuonekana mbele za
watu kuwa ndiye aliyefanya mambo makubwa wakati hamna kitu.
“Msibani maneno yalikuwa yanazungumzwa sana tena chini kwa chini
mwenyewe Wolper kainamisha kichwa chini kwa aibu asa sijui atazilipa
maana huyo mwenye nazo ni mbongo wa kawaida lakini si mtu wa njaa kama
sisi bongo movie,”
alisema.
Vichwa Vya Habari
Language
Friday, 11 January 2013
HABARI: MCHUNGAJI MTIKILA AFUFUA MAPYA KATIKA MCHAKATO WA KUTOA MAONI YA KATIBA MPYA
MAKUNDI maalumu jana yaliendelea kutoa maoni yao
kwenye mchakato wa Katiba Mpya, huku DP kikipendekeza Rais aapishwe
baada ya siku 90 tangu kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu.
Mbali na maoni hayo yaliyowasilishwa na Mwenyekiti
wa chama hicho, Mchungaji Christopher Mtikila, makundi mengine;
wakulima, wafugaji, wanahabari na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) nayo
yalijitokeza kutoa moyoni.Mtikila alisema kipindi hicho cha siku 90 kitatoa
fursa kwa watu wanaotaka kuwasilishapingamizi dhidi ya ushindi wa Rais
mteule kufanya hivyo, kabla ya kuapishwa.Alisema pingamizi linaweza
kufanyiwa kazi kwa kipindi hicho cha miezi mitatu ili kuhakikisha kuwa
taifa linapata kiongozi halali mwenye ridhaa ya wananchi.
“Pia tunataka kinga ya Rais ikome pale anapomaliza
muda wake wa uongozi, kama alifanya makosa yoyote ya jinai aweze
kushtakiwa ili kujenga nidhamu ya uongozi katika ofisi ya umma.
Utaratibu wa kumwondoa madarakani uimarishwe asisubiriwe hadi amalize
muda wake wa uongozi.”
Alisema kuwa Katiba ya nchi inapaswa kuwa mali ya
wananchi wenyewe ili watawala wasijihusishe katika kuwaundia wananchi
Katiba kama ilivyo kwa mchakato unaoendelea sasa wa kupata Katiba Mpya.
“Kumekuwa na hoja ya kuwapo kwa Serikali ya
Tanganyika, hilo ni jambo muhimu na watu kutoka Tanganyika ni lazima
wawe na Serikali yao ndani ya mipaka ya ardhi yao kupitia Katiba Mpya,”
alisisitiza Mchungaji Mtikila.
Aliongeza kuwa nafasi za wabunge wa viti maalumu
bungeni ziondolewe ili viti hivyo vishindaniwe kidemokrasia. Alisema
wanawake wanatakiwa waelimishwe na kupikwa ili wahimili ushindani katika
medani za kisiasa. Alisema kuwa taifa linahitaji viongozi bora na siyo
kustarehesha jinsia.
MICHEZO: NIGERIA KUSHINDA KOMBE LA MATAIFA YA AFRIKA 2013?
Wacheza kamali wanataka kucheza karata zao vizuri
kuhusu kinyang'anyiro cha ubingwa wa Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka
2013.
Wacheza kamali hao wataelekeza karata yao katika timu ya Nigeria
wakiipa nafasi ya kuwa katika timu tatu bora za juu.
Timu ya Nigeria, The Super Eagles, imeshiriki mara 16 katika mashindano ya kombe hilo na kushinda mara mbili, ikishika nafasi ya pili mara nne na mara saba katika nafasi ya tatu, ikiwa ni rekodi ya kujivunia katika kipindi cha miaka 50.
UN YAOMBA MSAADA WA KIJESHI MALI
Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, Susan Rice, alihoji ikiwa rais Dioncounda Traore alikuwa ametoa ombi maalum na kufafanua aina ya msaada anaotaka.
Ufaransa inatarajiwa kutoa jibu lake leo wakati wa mkutano wa dharura utakaofanyika , kwa mujibu wa balozi wa Ufaransa katika Umoja wa Mataifa, Gerard Araud.
Wapiganaji wa kiisilamu wameweka sheria kali za kiisilamu katika eneo hilo.
Kwa sababu ya mipango ya usafiri na vifaa , kikosi cha wanajeshi wa Afrika hakitatarajiwa kuanza kazi hadi ifikapo Septemba au Oktoba
BURUDANI: TRACK MPYA NA KALI KULIKO YA THE BATO-GET UR BODY BUSY
Kama ulikuwa humjui ni kati ya jamaa waliokuja kasi katika game ya muziki wa bongo flava na pia ni mwana muziki mwenye nyimbo nyingine kali ambazo pia utazipata kupitia hapa hapa www.bonmusic5.blogspot.com iliyotengenezwa na producer Stevee wa STREET SOUND RECORDS.
Subscribe to:
Posts (Atom)