Kama unakumbuka msanii Jackline Wolper alimpatia sh mil 16 Sajuki kwa ajili ya matibabu nchini India,
sasa yameanza kuibuka mengine ambapo inadaiwa kuwa kiasi hicho cha
fedha alichukua kwa mtu na mwenye nazo ameshindwa kuvumilia ameamua
kuanza kumdai ili azirudishe tofauti na makubaliano yalivyokuwa.
Inadaiwa kuwa habari hizo zilianza kuzuka tangu siku ambayo Sajuki
amefariki, huku mwenye fedha hizo akidai kuwa alitoa fedha hizo kwa
makubaliano kwamba atarudishiwa mapema lakini hadi muda waliopangwa
umepita haoni dalili zozote za kupewa fedha zake.
Chanzo kimoja cha kuaminika kilizungumza na mwandishi wetu kutoa story ilivyo, ambapo kilidai kuwa ishu hiyo imeanza kujitokeza
upya siku ya msiba na wenyewe walitaka kulipana kimya kimya lakini
baada ya maneno kuwa makubwa wamepanga kulipana muda wowote sasa.
Hata hivyo chanzo hicho kilisema kuwa Wolper hakutakiwa kutoa kiasi
chote cha pesa kwa Sajuki lakini alifanya hivyo ili kuonekana mbele za
watu kuwa ndiye aliyefanya mambo makubwa wakati hamna kitu.
“Msibani maneno yalikuwa yanazungumzwa sana tena chini kwa chini
mwenyewe Wolper kainamisha kichwa chini kwa aibu asa sijui atazilipa
maana huyo mwenye nazo ni mbongo wa kawaida lakini si mtu wa njaa kama
sisi bongo movie,”
alisema.
No comments:
Post a Comment