Rais wa zamani wa Zambia Rupiah Banda amesema hana hatia katika kesi
anayokabiliwa nayo ya kutumia vibaya mamlaka wakati wa kipindi chake cha
uongozi.
Mashtaka anayokabiliwa nayo Banda yamehusishwa na mkataba alioidhinisha
kati ya nchi hiyo na Nigeria kuhusu uuzaji wa mafuta ambao wendesha mashtaka
wanasema ulinuia kufaidi bwana Banda na familia yake.
"hapana bwana Jaji , nakanusha mashtaka ,'' Banda alimbia jaji.
Rais huyo wa zamani anasema kuwa mashtaka hayo ni sehemu ya njama za
kisiasa dhidi yake na washirika wake.
Baada ya miaka mitatu mamlakani, alishindwa na mpinzani wake Michael
Sata katika uchaguzi mwaka 2011, ingawa aliachiliwa kwa dhamana siku ya
Jumatatu.
Wendesha mashtaka wanasema kuwa Banda na mwanawe Henry Banda waliweka
pesa katika akaunti za kigeni, pesa zilizotokana na mkataba wa mafuta kati ya
Zambia na Nigeria. Pesa hizo inadaiwa zilitumika kufaidi familia ya Banda.
Henry Banda aliondoka nchini baada ya babake kushindwa kwenye uchaguzi
na anasakwa na polisi.
Serikali ya Sata imeanzisha uchunguzi dhidi ya washirika wakuu wa Banda
kufuatia madai ya kuhusika na ufisadi wakati wa utawala wa Banda.
Waziri mmoja wa zamani amepatikana na hatia na anajiandaa kukata rufaa
No comments:
Post a Comment