Vikosi vya uokoaji vinasema, watu wapatao 30 wamefariki dunia na mamia
wengine wanahofiwa kukwama baada ya jingo la ghorofa nane kuporomoka katika mji
mkuu wa Bangladesh, Dhaka.
Juhudi za ziada zinaendelea kuwaokoa watu walionaswa kwenye kifusi.
Watu wapatao 200 wamejeruhiwa kufuatia ajali hiyo. Jeshi linasaidia shughuli za
uokoaji katika eneo la tukio nje kidogo ya jiji la Dhaka.
Matukio ya majengo kuporomoka nchini Bangladesh ni ya kawaida kutokana
na majengo mengi marefu kujengwa kinyume na sheria za ujenzi.
Jengo lililoporomoka lilikuwa na kiwanda cha nguo, benki na maduka
kadhaa. Liliporomoka asubuhi wakati watu wakielekea makazini.
Watu wengi wamekusanyika karibu na eneo la tukio wakiwatafuta ndugu na
marafiki. Mwandishi wa BBC mjini Dhaka anasema haijafahamika kilichosababisha
jengo hilo kuporomoka, lakini vyombo vya habari nchini humo vimearifu kwamba,
nyufa zilionekana kwenye jengo hilo siku ya Jumanne.
Polisi wameviambia vyombo vya habari kwamba, waliona ghafla sehemu ya
nyuma ya jengo hilo ikianguka Jumatano asubuhi na baada ya muda mfupi jengo
lote likafuatia isipokua nguzo kuu na sehemu ya ukuta wa mbele hali
iliyosababisha taharuki.
Maafisa wanasema, ni sehemu ya chini pekee ya jengo hilo la Rana Plaza
ndio ilibakia imara baada ya kuporomoka, wakati wanajeshi na waokoaji wa idara
ya zimamoto wakiwa na vifaa vya kukatia vyuma na matingatinga wakifukua kifusi
ili kuwaokoa watu walionaswa .
Mkuu wa polisi wa eneo hilo, Mohammed Asaduzzaman, ameliambia shirika
la habari la AFP kwamba, hali ilikua mbaya sana.
Novemba mwaka jana, moto uliounguza kiwanda cha nguo nje ya jiji la Dhaka uliua watu 110 na kusababisha wananchi kupigia kelele kuhusu viwango vya usalama kwenye viwanda husika.
Novemba mwaka jana, moto uliounguza kiwanda cha nguo nje ya jiji la Dhaka uliua watu 110 na kusababisha wananchi kupigia kelele kuhusu viwango vya usalama kwenye viwanda husika.
Mara mwisho jengo la ghorofa nne liliporomoka jijini Dhaka mnamo mwaka 2010 na kusababisha vifo vya watu 25 na wengine kadhaa kujeruhiwa.
No comments:
Post a Comment