Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa linatarajiwa kupigia kura azimio
linalopendekeza kuundwa kwa kikosi cha kulinda amani nchini Mali.
Kikosi hicho chenye wanajeshi 12,600 kinajumuisha takriban wanajeshi
6,000 kutoka nchi za Magharibi mwa Afrika ambazo tayari zina wanajeshi wao
nchini humo.
Azimio hilo limependekezwa na Ufaransa ambayo iliingilia kati mzozo wa
Mali mnamo mwezi Januari ili kupambana na wapiganaji wa kiisilamu Kaskazini mwa
nchi hiyo.
Kikosi hicho kinatarajiwa kwenda Mali mwanzoni mwa mwezi Julai kabla ya
uchaguzi mkuu.
No comments:
Post a Comment