Rais Mstaafu wa Afrika Kusini Nelson Mandela amepelekea hospitalini
kufanyiwa uchunguzi wa kiafya.
Kwa muujibu wa tovuti ya Urais wa Afrika Kusini, Madaktari wanaomfanyia
uchunguzi Mzee Mandela wamesema hakuna haja ya kuwa na tahariku.
Kwa muda mrefu sasa hali ya kiafya ya rais huyo mstaafu imekuwa ni
swala la kutia wasiwasi.
Mandela mwenye umri wa miaka 94 alilazwa hospitalini kwa siku 18 mwezi
wa Desemba mwaka jana kutokana na kutatizwa na mapafu pamoja vijiwe ndani ya
kibofu chake cha mikojo.
Taarifa iliyoandikwa kwenye mtandao wa Ofisi ya Rais Jacob Zuma
zimeeleza kuwa Mzee Mandela alipelekwa katika Hospitali ya Mjini Pretoria kwa
uchunguzi wa kawaida wa ki-afya
Taarifa hiyo imeendelea kusima kuwa hatua hiyo imechukuliwa kutikana na
matatizo yanayoambatana na Umri wake mpevu.
Mzee Mandela alifudumu kama rais wa Afrika Kusini kati ya mwaka 1994 to
1999 na ndiye rais wa kwanza mweusi kuwahi kuitawala nchi hiyo.
Kutokana na juhudi zake za kupigania demokraisa na kupambana na sera za
ubaguzi wa rangi nchini humo, Mzee Mandela anatambulika kama Baba wa Taifa
nchini Afrika Kusini.
Tangu mwaka 2004 Mzee Nelson Mandela amekuwa hajitokeza hadharani au
kushiriki katika shughuli za umma.
Umri unAmsumbua
ReplyDeleteKweli kabisa, miaka 94 sio mchezo mtu wangu
Delete