Mwanajeshi mmoja wa Ufaransa nchini Mali ameuawa na wengine wawili
kujeruhiwa vibaya, kwa mujibu wa maafisa wa Ufaransa, mwanajeshi huyo kutoka
kikosi maalum cha Ufaransa aliuawa Magharibi mwa nchi baada ya gari lake
kulipukiwa na bomu lililokuwa limetegwa kando ya barabara.

Ufaransa ilitangaza kuanza kuondoa baadhi ya wanajeshi wake 4,000
walioko Mali.
Lakini wengine 1,000 watasalia nchini humo hadi mwakani kuweza
kukabiliana na wapiganaji wa kiisilamu walio na uhusiano na kundi la Al-Qaeda Baadhi ya miji, imeweza kudhibitiwa na wanajeshi hao, lakini wapiganaji
hao wangali kwenye maficho yao ya mwisho Kaskazini mwa Mali ambako wanafanya
mashambulizi ya kuvizia dhidi ya wanajeshi wa Mali na Ufaransa.
Hivi maajuzi Umoja wa Mataifa uliafikia kunda kikosi cha wanajeshi
12,000 kushika doria nchini Mali.