MJUMBE wa
Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) taifa, kupitia
Mkoa wa Arusha, Benson Mollel (26) amekutwa amefariki dunia ndani ya Hoteli ya
Lush Garden Business, iliyopo Mtaa wa Jacaranda katikati ya Jiji la
Arusha.
Mashuhuda wa tukio
hilo walisema Mollel alikutwa akiwa amekufa
jana mchana na kwamba tukio hilo
limezua hofu kwa wakazi wa Jiji la Arusha, huku wakijiuliza chanzo cha kifo
chake.
Kifo cha mwanasiasa
huyo mchanga ambaye pia alikuwa ni mfanyabiashara wa madini mkoani hapa,
kimezusha maswali mengi wakati wengine wakihusisha tukio hilo na masuala ya
kisiasa na upande mwingine wakidai ni masuala la kibiashara.
Hisia hizo zinatokana
na ukweli kwamba Arusha ni jiji lenye hekaheka za kisiasa hasa ndani ya CCM ambapo
Mollel alikuwa mmoja wa vinara wake.
Polisi waliwasili
hotelini hapo saa 8.00 mchana na kuupakia mwili wa marehemu kwenye gari na
kisha kuupeleka Hospitali ya Mount Meru kwa ajili ya kuhifadhiwa.
Mkuu wa Polisi wa
Wilaya wa Arusha (OCD), Gilles Muruta akizungumza katika eneo la tukio alisema:
“Tunachunguza tukio hili ambalo ni la ghafla.”
huyo mlo mwekea alama ya viringo sio yeye... yeye ni huyo wa katikati...
ReplyDelete