SIKU chache baada ya Rais Jakaya Kikwete kuwaagiza Polisi,wakuu wa mikoa
na wilaya kutofanya ajizi kwenye suala la wachochezi wa kidini , badala yake
wachukue hatua stahiki,baadhi ya wasomi na wanaharakati wamepinga kauli hiyo na
kudai ni maneno ya kisiasa.
Wamedai kuwa kuanzia Serikali ya Awamu ya Tatu hadi hii ya nne
zimekuwepo kauli za kupiga marufuku kashfa dhidi ya dini nyingine lakini
kukashifiana kumekuwa kukifanyika tena kwa uwazi bila hatua
kuchukuliwa.
Wakizungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti, walitoa mifano ya
kuwepo na mihadhara, CD, DVD na vipeperushi vya uchochezi na kashfa dhidi ya
dini lakini hakuna anayechukuliwa hatua.
Kwa kuwa mambo haya yamekuwa yakifanyika muda mrefu bila hatua kuchukuliwa wameshauri Polisi,wakuu wa mikoa,wilaya na usalama wa taifa wachukuliwe hatua kwa kushindwa kusimamia sheria na sasa amani ya nchi inaingia shakani.
Kwa kuwa mambo haya yamekuwa yakifanyika muda mrefu bila hatua kuchukuliwa wameshauri Polisi,wakuu wa mikoa,wilaya na usalama wa taifa wachukuliwe hatua kwa kushindwa kusimamia sheria na sasa amani ya nchi inaingia shakani.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk Benson Bana amesema kauli
aliyoitoa Rais Kikwete ni kauli ya kisiasa na alitakiwa kutoa tamko
la kuwawajibisha watendaji wake pindi wanaposhindwa kutekeleza wajibu
wao.
Alisema vitendo hivi vyote vya machafuko ya kidini vinafanyika
hadharani huku wakuu wa mikoa,wilaya na Usalama wa taifa
wakishuhudia wakati jukumu la kulinda amani katika eneo husika ni lao.
Naye Naibu Katibu Mkuu Bara wa Chama Cha Wananchi (CUF), Julius
Mtatiro anasema Serikali inayoongozwa na CCM haina uwezo wa kutokomeza udini.
Katika hotuba yake ya kawaida ya kila mwisho wa mwezi aliyoitoa
Februari 28, mwaka huu, Rais Kikwete aliiagiza Polisi nchini kukamilishe mapema
upelelezi wa makosa ya vurugu za kidini na wahusika wafikishwe haraka kwenye
vyombo vya sheria ili iwe fundisho kwa wengine.
Aliwataka wakuu wa mikoa nao kutoona ajizi katika hilo.
No comments:
Post a Comment