Hii leo
wakenya wanapiga kura katika uchaguzi wa kihistoria chini ya katiba
mpya. Foleni tayari zimeanza kushuhudiwa katika vituo.
Kinyang'anyiro ni kikali kati ya Muungano wa Cord na Jubilee wa Raila Odinga na
Uhuru Kenyatta.
Kwenye ukurasa huu tutakupasha matukio kila yanapojiri hadi upigaji kura utakapokamilika mwendo wa saa kumi na moja jioni.
08:43 Mgombea wa urais wa muungano wa CORD, waiziri mkuu Raila Odinga anatarajiwa kupiga kura yake wakati wowote kuanzia sasa
08:30 @smugera anasema kwamba kupiga kura kunachukua takriban dakika 12 minutes. #bbcnewsday
08:25 Hassan Majid pia mwandishi wa BBC anasema
kuwa polisi wamepata mwili mmoja wa mtu aliyeuawa na mwingine kujeruhiwa
kwa kukatwa panga katika eneo la Moshomoroni
08:24 Mwandishi wa BBC mjini Mombasa, Karen
Allen anasema kuwa polisi wamepata maiti za polisi wanne ambao wameuawa
katika eneo la eneo la Changamwe , Kaskazini mwa Mombasa. Hana taarifa
zaidi kwa sasa
08:16:Frawaso Kimutai kupitia
Bofya
facebook yuko katika kituo cha Menengai mjini Nakuru kura
ilianza kupigwa saa moja asubuhi na foleni ni ndefu ingawa inakwenda
polepole mwendo wa kobe
08:15: Fatma Sanbur yuko mtaani Kibera na
anasema watu ni wengi sana lakini hakuna mbinu ya kupanga foleni.
Anasema watu wanapangwa kwa orodha ya majina na hata baada ya saa moja
tangu waanza kupangga foleni saa kumi na moja, shughuli yab upigaji kura
ilikuwa haijaanza
07:11 James Mwangi: Kwenye ukurasa wa Facebook wa
Bofya
bbcswahili anasema yuko kwenye foleni na habanduki
07:14 Hison Nyakundi : Yuko mjini Eldoret kwa Foleni tayari kupiga kura
Bofya
bbcswahili
07:24 Kips Oscar: Kupitia Facebook yuko katika
kaunti ya Marsabit anasema upigaji kura unaendelea bila wasiwasi na kuwa
wanatarajia shughuli itakamilika kwa muda bila wasiwasi
07:28: Mgombea mwenza wa Uhuru Kenyatta, William Ruro amepiga kura mjini Eldoret
07:32: William Ruto anasema kuwa anajivunia
uchaguzi wa Kenya unafanyika kwa amani licha ya dukuduku la wengi.
Anasema anawataka wapinzani kukubali matokeo ya uchaguzi vyovyote
matokeo hayo yatakavyokuwa.
07:43 Upiga kura bado haujaanza katika baadhi ya
sehemu za Kenya. Wapiga kura wanalalamika kuwa katika vituo kadhaa
tarakilishi zimegoma na kwa hivyo watasubiri muda kabla ya kupiga kura
zao
07:47 Eco Seyar Papa akiwa mjini Nairobi anasema
Wakenya wamejitokeza kwawingi jijini Nairobi katika eneo la Dagoreti.
Foleni zilianza kupigwa kuanzia saa tisa usiku tangu kuanzishwa kwa
demokirasia ncini Kenya watu waeneo hili hawajawai kujitokeza kwa
mapenzi kama inavyo onekana.
07:50 Mwandishi wa BBC Ann Mawathe yuko mjini
Kisumu na anasema ameona foleni ndefu sana watu wakiwa hamasa kupiga
kura. Wamepiga foleni tangu saa nane usiku.
07:52 Mombasa eneo la Kaloleni mpiga kura mmoja
amesema hadi kufikia sasa upigaji kura haujaanza kwani maafisa wa tume
ya uchaguzi bado hawajawasili na vifaa vyao
No comments:
Post a Comment