Vichwa Vya Habari
Language
Monday, 21 January 2013
MICHEZO: LUKAKU: "SIRUDI TENA CHELSEA"
ROMELU LUKAKU ametangaza rasmi kuwa hana nia ya
kurejea tena katika klabu yake ya Chelsea ikiwa atakuwa miongoni mwa
wachezaji wake wa ziada.
Lukaka amesema yuko tayari kuendelea kuichezea West Brom kwa mkopo msimu ujao.Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 19 aliifungia West Brom bao lake la pekee na kuipa timu yake ushindi wake wa kwanza msimu huu.
HABARI: MATEKA 37 TOKA NCHI 8 WALIUAWA ALGERIA
Waziri mkuu wa Algeria Abdelek Sellal amesema mateka
37 wa kigeni kutoka nchi 8 za kigeni waliuawa katika makabiliano ya
watekaji nyara na jeshi.
Katika taarifa yake wazieri mkuu alisema kuwa
raia mmoja wa Canada ni miongoni mwa wapiganaji walioteka kiwanda cha
gesi na kuwakamata mateka.Alisema kuwa watekaji nyara 29 waliuawa na wengine watatu walikamatwa wakiwa hai.
Tukio hilo lilifika kikomo siku ya Jumapili . Inaaminika mateka zaidi ya 45 wakiemo raia wa Algeria waliuawa.
Wanajeshi wanaendelea na upekuzi katika eneo kulipotokea utekaji nyara katika kiwanda cha mafuta cha Amenas. Ndani ya kiwanda hicho zaidi ya maiti ishirini zilizoteketea kiasi cha kutoweza kutambulika zilipatikana.
Taarifa zaidi zinaarifu kuwa Maiti za mateka kutoka Japan, Norway, Uingereza, Marekani na Malaysia bado hazijatambuliwa huku maafisa wa usalama wakisema kuwa watekaji nyara watano tayari walithibitishwa kuuawa na wapiganaji.
HABARI: AFARIKI KWENYE AJALI NA ZAIDI YA TSH. MILIONI 13 KWENYE SOKSI ALIYOKUWA AMEVALIA KIATU
Abiria mmoja amefariki papohapo huku akiwa na zaidi ya Sh13
milioni mfukoni, wengine 48 wamejeruhiwa mkoani Mbeya baada ya basi
walilokuwa wakisafiria kuacha njia na kupinduka.
Wakati ajali hiyo ikitokea Mbeya, Dar es Salaam
watu wawili wamefariki dunia baada ya mabasi ya daladala kugongana
maeneo ya Kongowe, nje kidogo ya Dar es Salaam.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Engelbert Kiondo
alisema ajali hiyo ilisababishwa na mwendokasi wa magari hayo
yaliyokuwa yanashindana.
Majeruhi 12 walipelekwa Hospitali za Temeke na Muhimbili kwa matibabu.
Katika ajali ya Mbeya, basi hilo ambalo ni mali ya Kampuni ya Nganga Express ilitokea jana asubuhi eneo la Inyala, Wilaya ya Mbeya Vijijini.
Basi hilo lilikuwa likitokea Mbeya kwenda Dar es Salaam.
Katika ajali ya Mbeya, basi hilo ambalo ni mali ya Kampuni ya Nganga Express ilitokea jana asubuhi eneo la Inyala, Wilaya ya Mbeya Vijijini.
Basi hilo lilikuwa likitokea Mbeya kwenda Dar es Salaam.
Dereva wa basi hilo, Alex Bunyinyiga alisema
wakati akiendesha basi hilo, alipofika kwenye mteremko wa Inyara, mahali
ambapo kuna kona kali, aliona lori lililokuwa limeegeshwa upande wa
kulia wa barabara.
Bunyinyiga alisema alipolikaribia lori hilo,
ghafla lilitokea gari lingine aina ya Fuso ambalo lilipita lori
lililoegeshwa na kumfuata upande wake, hali ambayo ingesababisha
kugongana uso kwa uso.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Diwani Athumani
alimtaja mtu aliyepoteza maisha katika ajali hiyo kuwa ni Enock Lwila,
mkazi wa Mama John, mjini Mbeya.
Diwani alisema Lwila wakati akipatwa na ajali
alikuwa na Sh13 milioni mfukoni ambazo ziliokolewa na polisi waliowahi
eneo la tukio. Diwani alisema kwa sasa fedha hizo ziko salama
mikononi mwa polisi na kwamba, baada ya kupatikana nduguwatakabidhiwa.
HABARI: MUASI WA NIGERIA AMEKAMATWA AFRIKA KUSINI
Mahakama nchini Afrika Kusini imempata na hatia ya vitendo vya kigaidi kiongozi wa waasi wa Nigeria Henry Okah.
Okah alipatikana na hatia ya makosa 13 kuhusiana na vitendo vya kigaidi.
Alikanusha makosa hayo ingawa kundi analoongoza la Mend, lilikiri kutekeleza mashambulizi hayo.
Jaji wa mahakama kuu mjini Johannesburg, Neels Claassen, alimpata na hatia Okah ya makosa ya kupanga njama ya mashambulizi pamoja na kufanya vitendo vya kigaidi ikiwemo kulipua mabomu.
"ushahidi ambao ulitolewa na washirika wake haukupingana,'' alisema jaji Claassen
Okah alikamatwa kwa kosa la kumiliki bunduki kinyume na sheria nchini Angola mwaka 2007 na kisha kuhamishwa hadi nchini Nigeria ingawa hakuwahi kuhukumiwa.
Aliachiliwa baada ya miaka miwili chini ya msamaha uliotolewa kwa wapiganaji walio katika maeneo ya mafuta na ndipo aliporejea Afrika Kusini ambako aliishi hadi mwaka 2003.
Subscribe to:
Posts (Atom)