Abiria mmoja amefariki papohapo huku akiwa na zaidi ya Sh13
milioni mfukoni, wengine 48 wamejeruhiwa mkoani Mbeya baada ya basi
walilokuwa wakisafiria kuacha njia na kupinduka.
Wakati ajali hiyo ikitokea Mbeya, Dar es Salaam
watu wawili wamefariki dunia baada ya mabasi ya daladala kugongana
maeneo ya Kongowe, nje kidogo ya Dar es Salaam.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Engelbert Kiondo
alisema ajali hiyo ilisababishwa na mwendokasi wa magari hayo
yaliyokuwa yanashindana.
Majeruhi 12 walipelekwa Hospitali za Temeke na Muhimbili kwa matibabu.
Katika ajali ya Mbeya, basi hilo ambalo ni mali ya Kampuni ya Nganga Express ilitokea jana asubuhi eneo la Inyala, Wilaya ya Mbeya Vijijini.
Basi hilo lilikuwa likitokea Mbeya kwenda Dar es Salaam.
Katika ajali ya Mbeya, basi hilo ambalo ni mali ya Kampuni ya Nganga Express ilitokea jana asubuhi eneo la Inyala, Wilaya ya Mbeya Vijijini.
Basi hilo lilikuwa likitokea Mbeya kwenda Dar es Salaam.
Dereva wa basi hilo, Alex Bunyinyiga alisema
wakati akiendesha basi hilo, alipofika kwenye mteremko wa Inyara, mahali
ambapo kuna kona kali, aliona lori lililokuwa limeegeshwa upande wa
kulia wa barabara.
Bunyinyiga alisema alipolikaribia lori hilo,
ghafla lilitokea gari lingine aina ya Fuso ambalo lilipita lori
lililoegeshwa na kumfuata upande wake, hali ambayo ingesababisha
kugongana uso kwa uso.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Diwani Athumani
alimtaja mtu aliyepoteza maisha katika ajali hiyo kuwa ni Enock Lwila,
mkazi wa Mama John, mjini Mbeya.
Diwani alisema Lwila wakati akipatwa na ajali
alikuwa na Sh13 milioni mfukoni ambazo ziliokolewa na polisi waliowahi
eneo la tukio. Diwani alisema kwa sasa fedha hizo ziko salama
mikononi mwa polisi na kwamba, baada ya kupatikana nduguwatakabidhiwa.
No comments:
Post a Comment