Waziri mkuu wa Algeria Abdelek Sellal amesema mateka
37 wa kigeni kutoka nchi 8 za kigeni waliuawa katika makabiliano ya
watekaji nyara na jeshi.
Katika taarifa yake wazieri mkuu alisema kuwa
raia mmoja wa Canada ni miongoni mwa wapiganaji walioteka kiwanda cha
gesi na kuwakamata mateka.Alisema kuwa watekaji nyara 29 waliuawa na wengine watatu walikamatwa wakiwa hai.
Tukio hilo lilifika kikomo siku ya Jumapili . Inaaminika mateka zaidi ya 45 wakiemo raia wa Algeria waliuawa.
Wanajeshi wanaendelea na upekuzi katika eneo kulipotokea utekaji nyara katika kiwanda cha mafuta cha Amenas. Ndani ya kiwanda hicho zaidi ya maiti ishirini zilizoteketea kiasi cha kutoweza kutambulika zilipatikana.
Taarifa zaidi zinaarifu kuwa Maiti za mateka kutoka Japan, Norway, Uingereza, Marekani na Malaysia bado hazijatambuliwa huku maafisa wa usalama wakisema kuwa watekaji nyara watano tayari walithibitishwa kuuawa na wapiganaji.
No comments:
Post a Comment