KAMATI ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetoa adhabu ya kuvifungia muda wa miezi sita vituo viwili vya redio za dini, Imani na Kwa Neema kwa kile kilichoelezwa ni kuendesha vipindi vya uchochezi.
Vilevile kamati hiyo imetoa adhabu ya faini
ya Sh5 milioni kwa Kituo cha redio cha Clouds FM baada ya kubainika pia
kukiuka taratibu za utangazaji kwa kurusha hewani kipindi
kilichotafsiriwa kuwa ni cha uchochezi.
Kamati hiyo ya maudhui ilitangaza adhabu hizo
jana jijini Dar es Salaam mbele ya waandishi wa habari ikisisitiza kuwa
lengo lao ni kuhakikisha kuwa vyombo vya habari vinazingatia maadili.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui ya
TCRA,Walter Bugoya alisema TCRA imefikia hatua hiyo baada ya kuyafanyia
uchunguzi wa kina malalamiko yaliyotolewa na wasikilizaji wa vituo hivyo
vya redio.
Bugoya alisema redio hiyo ilitangazia
wasikilizaji wake wasishiriki kwenye mkakati huo wa Sensa ya Taifa kwa
kile walichodai kulingana na imani ya Kiislamu, wasingejua hatima ya
mkakati huo.
Kuhusu Redio Kwa Neema inayorusha matangazo
yake kutokea Geita, Bugoya alisema ilieneza uchochezi dhidi ya mtafaruku
wa kidini uliozuka mkoani humo juu ya upande gani una haki ya kuchinja
wanyama kwa ajili ya kitoweo.
Akizungumzia Kituo cha redio cha Clouds,
Buyoga alisema kamati imeitaka kulipa fidia ya Sh5 milioni baada ya
kubainika kuwa nacho kilienda kinyume cha maadili ya utangazaji kupitia
kipindi chake cha Power Break Fast, cha Jicho la Ng’ombe walitoa kauli
za uchochezi.
No comments:
Post a Comment