Baada ya sakata la kufariki ghafla mbunge wa chama tawala NRM nchini
Uganda,rais Museveni pamoja na waziri wa ulinzi na mkuu wa majeshi
wamekuwa wakitoa kauli za kutishia kuliachia jeshi lichukue uongozi
nchini humo.
Nchini Uganda baada ya sakata la wiki kadhaa la kufariki ghafla mbunge
wa chama tawala NRM na aliyekuwa mkosoaji mkubwa wa serikali ya chama
chake inayoongozwa na Museveni Selina Nambanda,sasa rais pamoja na
waziri wa ulinzi na mkuu wa majeshi katika nyakati tofauti wamekuwa
wakitoa kauli za kutishia kuliachia jeshi lichukue uongozi nchini
Uganda. Yote yanatokana na mpasuko ndani ya chama cha NRM ambapo wabunge
wa chama hicho wamekuwa wakitaka ianzishwe tume huru ya kuchuguza kifo
hicho,hatua ambayo inapingwa na rais Museveni.Wabunge kadhaa wameshatiwa
ndani kufuatia hoja hiyo.Kinachowatia wengi mashaka kwa sasa ni kauli
hizo za kutaka jeshi liidhibiti serikali, Saumu Mwasimba amemuuliza
mchambuzi wa masuala ya kiasiasa,mhadhiri wa masuala ya sheria katika
chuo kikuu cha Makerere,Dkt John Nsokwa anaitazama vipi hatua hii.
Kusikiliza mazungumzo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.
No comments:
Post a Comment