Language

Wednesday, 23 January 2013

HABARI: HAYA NDIO MATOKEO YA UCHAGUZI ISRAEL

Wapiga kura wa Israel wamemuondowa patupu waziri mkuu Netanyahu anaekabiliwa na kazi ngumu kuweza kuunda serikali ya muungano 

Waisraeli wamepiga kura jana, na wamezusha maajabu. Mtangazaji wa zamani wa televisheni, Jair Lapid na chama chake cha kiliberali - Yesh Atid - amemaliza nafasi ya pili akijikingia viti 19 vya bunge la Knesset. Yeye ndiye mshindi mkubwa wa uchaguzi huo. Waziri mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, ameondolewa patupu na wapiga kura. Muungano wa vyama vya mrengo wa kulia vya Likud na Beitenu, anaouongoza, umejipatia viti 31 toka jumla ya viti 120 vya bunge la Israel - Knesset.
Baada ya ushindi kama huo, kimsingi mshindi hupanda ndani ya gari la fakhari

HABARI:WATU 23 WAMEUAWA NIGERIA KATIKA MASHAMBULIZI TOFAUTI

Washukiwa wa kundi la wapiganaji wa kiisilamu , wamelaumiwa kwa mauaji ya watu 23 katika mashambulizi tofauti Kaskazini mwa Nigeria
.
Walio shuhudia mauaji hayo wanasema kuwa washambuliaji waliwalenga watu waliokuwa wanauza nyama ya wanyamapori, katika eneo la Damboa siku ya Jumatatu na kuwaua watu 18.
Watu wengine watano walifariki Jumanne wakati kundi la wanaume waliokuwa wanacheza mchezo wa kamari walishambuliwa mjini Kano.
Kundi la Boko Haram, linalopigana kutaka kuweka sheria za kiisilamu, nchini Nigeria limekuwa likifanya mashambulizi, katika sehemu kadhaa nchini humo.
Boko Haram imelaumiwa kwa vifo vya takriban watu 1,400,

HABARI: SASA NI ZAMU YA CHADEMA KUIRARUA CCM

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimejibu CCM kuhusu kauli zake za hivi karibuni kuwa Chadema itakufa.Akihutubia Mwanza hivi karibuni, Nape Nnauye alikaririwa akisema Chadema itakufa kutokana na laana ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere na kwamba ni chama kilichojaa ubaguzi.
Akijibu kauli hiyo jana, Mkurugenzi wa Operesheni na Mafunzo wa Chadema, Benson Kigaila alisema chama hicho hakiwezi kulumbana na Nape.
Kigaila alisema Chadema haina makundi na haitakufa kwa laana ya Mwalimu Nyerere.
Tunataka kuwaambia kuwa Chadema haina ubaguzi hivyo haiwezi kufa leo wala kesho mpaka iwe imetimiza kazi yake ya kuwakomboa Watanzania. Kama ni suala la Mwalimu Nyerere, laana hiyo iko ndani ya CCM yenyewe,” alisema.
Akitaja sababu za kudai kuwa laana imo ndani ya CCM, Kigaila alisema chama hicho kimevunja umoja wa kitaifa uliojengwa na Mwalimu Nyerere na kwamba, alitunga kitabu kuwa CCM imeoza na kinanuka rushwa.
Aliongeza kuwa CCM ina laana ya Mwalimu kwa sababu imerasimisha ubaguzi kwa viongozi wanachama wao.
Ni haohao CCM wanaosema Chadema kina ukabila waliomzushia Dk Salim Ahmed Salim uongo kuwa ni Mwarabu na alihusika na kifo cha aliyekuwa mmoja wa waasisi wa taifa hili, Abeid Karume. Uchafu uliofanywa na wanamtandao,” alisema Kigaila.
Aliendelea kuituhumu CCM kwa kukandamiza haki za wafanyakazi, huku akitoa mfano wa tukio la kutekwa na kuteswa kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania (Mat), Dk Steven Ulimboka.
Pia, alitoa mfano wa wazee waliostaafu Jumuiya ya Afrika Mashariki ambao wanaodai mafao yao hadi leo, wakati Serikali ya Uingereza ilishalipa fedha zao tangu jumuiya ilipokufa mwaka 1977.
Kuhusu hatua ya kuwavua uanachama, baadhi ya viongozi wa Baraza la Vijana wa Chadema (Bavicha), Kigaila alisema chama hicho hakitavumilia makosa kama uzembe, ufisadi, udhaifu, ubadhirifu na usaliti.

Amshukia Mwigulu Nchemba
Pia, Kigaila alimshambulia Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Mwigulu Nchemba kwa madai kuwa, tuhuma alizotoa dhidi ya Chadema kwamba kinapanga mauaji, zinaidhalilisha Serikali na polisi.
Alimtaka Nchemba kupeleka ushahidi wa tuhuma zake kwenye vyombo vya sheria badala ya vyombo vya habari. “Tunataka kumwambia Rais Jakaya Kikwete, Mkuu wa Polisi, Said Mwema na Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa, Othman Rashid kuwa ukimya wao... ni tafsiri kuwa polisi sasa inafanya kazi kwa kufuata amri za Chadema,” alisema Kigaila.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...