Wapiga kura wa Israel wamemuondowa patupu waziri mkuu Netanyahu anaekabiliwa na kazi ngumu kuweza kuunda serikali ya muungano
Waisraeli wamepiga kura jana, na wamezusha maajabu. Mtangazaji wa zamani
wa televisheni, Jair Lapid na chama chake cha kiliberali - Yesh Atid -
amemaliza nafasi ya pili akijikingia viti 19 vya bunge la Knesset. Yeye
ndiye mshindi mkubwa wa uchaguzi huo. Waziri mkuu wa Israel, Benjamin
Netanyahu, ameondolewa patupu na wapiga kura. Muungano wa vyama vya
mrengo wa kulia vya Likud na Beitenu, anaouongoza, umejipatia viti 31
toka jumla ya viti 120 vya bunge la Israel - Knesset.
Baada ya ushindi kama huo, kimsingi mshindi hupanda ndani ya gari la
fakhari
. Yair Lapid lakini hakutaka makubwa na badala yake ameamua
kupanda teksi kutoka nyumbani kwake kwenda katika ukumbi wa sherehe
zilizoandaliwa na chama chake.Mshindi halisi wa uchaguzi huo Yair Lapid
anasema:"Taifa la Israel linakabiliwa na changamoto kubwa. Inabanwa na
mgogoro wa kiuchumi ambao ni kitisho kwa watu wa tabaka la wastani.
Israel inakumbwa na kitisho cha kutengwa kimataifa. Njia ni moja tu
kuweza kuzishinda changamoto hizo; Ushirikiano na mshikamano."
No comments:
Post a Comment