Language

Wednesday, 13 February 2013

MICHEZO: HILI NDILO BASI LILILOTOLEWA NA TBL MAALUMU KWA TIMU YA TAIFA STARS



HABARI MUHIMU: AHUKUMIWA KUNYONGWA HADI KUFA MBEYA

Mahakama kuu kanda ya Mbeya imemhukumu PETER MWAFRIKA mkazi wa Ndolezi wilayani Mbozi kunyongwa hadi kufa baada ya kupatikana na hatia ya kuua kwa kukusudia.



Akisoma hukumu hiyo iliyochukua saa 1.30 Jaji mfawidhi wa mahakama kuu kanda ya mbeya NOEL CHOCHA amesema licha ya mikono ya mahakama kufungwa kutoa adhabu ndogo kwa kosa la maauaji ya kukusudia, pia adhabu hiyo ni hatua ya kukomesha watu wenye tabia kama za mtuhumiwa kujichukulia hatua mikononi mwao.
Akirejea mazingira ya kesi hiyo jaji Chocha amesema mnamo Februaly 11,2010 Mshatakiwa na wenzake watatu walifanya kosa la mauaji ya kukudia chini ya kifungu 196 chasheria ya

mwenendo wa makosa ya jinai kwa kumuua KOSAM MWAFRIKA ambaye ni kaka wa marehemu katika kijiji cha Shaji kwa kumkata koromeo na kulitenganisha vipande viwili.
Jaji Chocha katika maelezo yake alisema mshtakiwa akiwa na wenzake ambao walitoweka baada ya mauaji hayo walimvamia Kosam akiwa na mkewe shambani

MICHEZO: MATOKEO NA RATIBA YA MECHI KUBWA ZA LEO DUNIANI


HABARI PICHA: MGAWANYIKO UNASHIKA KASI TANZANIA, HIZI NDIO BUTCHER ZA WAKRISTO


HABARI MUHIMU TOKA GPL: FREEMASONS WAUTEKA MJI WA MOSHI

IMANI ya jamii ya siri ya Freemasons imeonekana kuuteka Mji wa Moshi na vitongoji vyake kutokana na matangazo mengi kubandikwa kila kona yakihamasisha wafuasi kujiunga huku ofa ya utajiri ikipewa kipaumbele.

Risasi Mchanganyiko limeshuhudia matangazo mengi yanayohamasisha kujiunga na imani hiyo yakiwa yamebandikwa kila kona ya mji huu ikiwemo katika nguzo za umeme
Katika tangazo hilo, wahusika wameeleza kwamba watakaojiunga mapema watapewa magari ya kifahari na nyumba za kisasa ikiwa ndiyo njia za awali za kubadilisha maisha yao.
Mwandishi wetu alijifanya anataka kujiunga na kupiga namba za simu zilizowekwa katika tangazo hilo ambazo ni 0783 127 967 ambapo ilipokelewa na mwanaume aliyekataa kutaja jina lake lakini alitoa masharti ya kujiunga.
“Tuma majina yako matatu; lako, baba na babu yako halafu tuma na shilingi 100,000 kwenye namba 0714 084 841 ambayo ni ada ya uanachama kisha utakwenda Kindoroko Hotel, chumba namba 87 hapo utakutana na bosi wangu na utaandikishwa rasmi na kupewa nguo zenye nembo yetu,” alisema mtu huyo.

Mwandishi wetu alifika katika Hoteli ya Kindoroko iliyopo mjini hapa juzi, Jumapili Februari 10, mwaka huu, akaonana na mtu wa mapokezi na kujitambulisha kama mwanachama mpya anayetaka kuonana na mhusika aliyepanga chumba namba 87.
Cha kushangaza, mhudumu alimwambia hawana mteja wa aina hiyo katika hoteli yao na kwamba hakuna chumba chenye namba aliyoelekezwa, jambo lililoonesha wazi kuwa wahusika ni matapeli wanaotaka kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu.
Naye meneja wa hoteli hiyo aliyejitambulisha kwa jina moja la Sara alipopigiwa simu, alitoa majibu kama ya mtu wa mapokezi.
Upekuzi wa gazeti hili umebaini kuwa, simu namba 0714 084841 iliyotakiwa kutumiwa fedha na mtu aliyejiita wa Freemasons imesajiliwa kwa jina la Flora Tuvana.
 

TAARIFA YA KIFO CHA MSANII WA TMK WANAUME HALISI 'BK'


HABARI MUHIMU-OLE WAO WANAWAKE WAVUTAJI WA SIGARA

Wataalamu wa afya wanasema kuwa wanawake barani Ulaya wanafariki zaidi kutokana na saratani ya mapafu kuliko saratani ya matiti.

 

Wanaelezea kuwa saratani ya mapafu ndio imekuwa sasa saratani nambari moja ambayo inasababisha vifo miongoni mwa wanawake.
Hali hii tayari inashuhidiwa nchini Uingereza na Poland.
Kulingana na watafiti, hii ni ishara ya idadi kubwa ya wanawake wanaovuta sigara hali iliyoanza kujitokeza kuanzia mapema miaka ya tisini na sabaini.
Idadi ya vifo vinavyotokana na saratani ya mapafu, vitaendelea kuongezeka katika miaka ijayo, lakini sasa kwa sababu ya vijana wa kike wasiovutiwa na kuvuta sigara na ambao idadi yao sio kubwa sana , huenda vifo hivyo vikapungua.
Mwaka 2013, takriban wanawake 82,640 barani Ulaya watafariki kutokana na saratani ya mapafu ikilinganishwa na wanawake 88,886 watakaofariki kutokana na saratani ya matiti.
Wanatarajiwa kuwa vifo vinvyotokana na saratani ya mapafu kupungua mwaka 2020 au 2025 kwa sababu angalu vijana wa kiike hawavuti sana sigara.
Lakini ifikapo mwaka 2015, wanawake wengi watafariki kutokana na saratani ya mapafu kuliko saratani ya matiti, kulingana na mtaalamu wa afya ya wanawake, Profesa Carlo La Vecchia .
Takwimu zinaonyesha kuwa ingawa watu wengi zaidi wanaugua saratani, kwa sababu wanaishi muda mrefu zaidi,
ni watu wachache sana wanafariki kutokana na saratani.

Licha ya kupungua kwa idadi ya watu wanaofariki kutokana na saratani barani humo, idadi ya wanawakewanaofariki kutokana na saratani ya mapafu inaongezeka katika nchi zote za Ulaya.
Profesa La Vecchia,wa chuo kikuu cha Milan, Italy, anasema kuwa hali hii inaleta wasiwasi kwa sababu hakuna dalili kuwa ugonjwa huo unapungua.
Uvutaji sigara pamoja na ugonjwa wa sukari ndio vinachangia kuongezeka kwa ugonjwa huu. Lakini wataalamu wanasema bado hawajui nini kinasababisha sehemu kubwa ya saratani hiyo.
Wataalamu wanasema kuna umuhimu wa wanawake kuwacha kuvuta sigara

BURUDANI: N'SYNC-THIS I PROMISE LYRICS

"This I Promise You"
Ohh ohh...

When the visions around you,
Bring tears to your eyes
And all that surround you,
Are secrets and lies
I'll be your strength,
I'll give you hope,

BURUDANI: TID NAYE KWENDA BIG BROTHER AFRICA



Baada ya jana kusikia kuwa q chifu kachukua form TID nayeye naye kachukua form ya kushiriki big brother  na kufiksha idadi ya wasanii wa ongo kuwekahistoria ya kuchukua form za big brother ambako wema sepetu na nyeye aliichukua q cheaf na hemed pia wato kwenye nia ya kubeba kitita cha dola za kimarekani 300,000
Mshiriki wa mwaka jana Julio aliongea nakusema mtu kama TID angefaa sana kushiriki shindano hilo maana ni mcheshi na ana vigezo vingi vitavyomuwezesha kushinda.

BURUDANI: KUNDI LA MUZIKI LA PAH ONE LAMONG'ONYOKA!!!

Kundi ambalo lilikuwa linaundwa wasanii wanne kwa pamoja likiitwa Pah One sasa limevunjika kwani First Lady wa kundi hilo la Pah One mwanadada Aika ametangaza kujitoa rasmi kwenye kundi hilo pamoja na rapper na producer wa kundi hilo Nahreel na hivyo kundi hilo kubakiwa na wasanii wawili tu. Aika amesema kuwa sababu ya kumfanya ajitoe kwenye kundi hilo ni kutokuwa na maelewano mazuri ndani ya kundi hilo na kuongeza kwa kusema Nahreel ni Solo Artist hivyo yeye na Nahreel hawajavunja kundi hilo na si kwamba mapenzi yake yeye na Nahreel ndiyo sababu iliyopelekea kuvunjika kwa kundi hilo. Nahreel na Aika wanatarajia kuachia ngoma yao ya kwanza wakiwa kama Solo Artists tarehe 14 mwezi huu.

KIBONZO


HABARI MUHIMU: WIFI ANG'ATWA ULIMI MPAKA KUKATIKA

MWALIMU wa Shule ya Msingi Mfaranyaki iliyopo Manispaa ya Songea, Theresia Fuli anashikiliwa na polisi kwa kosa la kumjeruhi kwa kumng’ata ulimi hadi kukatika wifi yake kwa wivu wa mapenzi.

Akizungumza kwa tabu na gazeti hili jana kwenye hospitali ya mkoa alikolazwa wodi daraja la kwanza kwa ajili ya matibabu, majeruhi huyo Oliga Msigale mkazi wa Msamala amesema, bado ana maumivu makali ya ulimi ingawa amepatiwa matibabu.
Amesema siku ya tukio alishangaa kuona anavamiwa na wifi yake ambaye ni mtalaka wa kaka yake, ambapo alimtupia mtoto mkubwa wa kaka yake maharage ya moto kisha kumvamia yeye, huku akimtuhumu kuwa ndiye binti ambaye amechukua nafasi yake bila kujua kuwa yeye ni ndugu wa mume na alipoanguka chini alikabwa koo na alipotoa ulimi nje mwanamke huyo bila huruma alimngata ulimi na kutoa kipande cha ulimi kisha akatoroka eneo hilo.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...