Vichwa Vya Habari
Language
Friday, 25 January 2013
BURUDANI: LULU KUENDELEA KUSOTA SELO,NI BAADA YA DHAMANA YAKE KUPIGWA KALENDA
Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imesogeza mbele tarehe ya
usikilizwaji wa maombi ya dhamana ya msanii wa fani ya maigizo,
Elizabeth Michael, maarufu kama Lulu, anayekabiliwa na kesi ya kuua bila
kukusudia.
HABARI: KESI YA SISTA ALIYEFUMANIWA NA MUME WA MTU SUMBAWANGA KUSIKILIZWA TAREHE 29
KESI ya madai inayomkabili aliyekuwa Mtawa wa Shirika la
Kitawa la Kanisa Katoliki Jimbo la Sumbawanga, Sista Yasinta Sindani
anayedaiwa kufumaniwa na mume wa mtu imepangwa kusikilizwa Januari 29
mwaka huu.
“Sista’ Yasita licha ya kuwa mtumishi wa afya
katika Hospitali ya Mkoa wa Rukwa mjini hapa lakini inadaiwa
ameachana na maisha ya kitawa miaka miwili iliyopita kwa hiyari
yake akiwa Mtawa wa Shirika la Masista wa Maria Mtakatifu Malkia wa
Afrika (MMMA).
Shauri hilo la madai linatarajiwa kuanza
kusikiliza katika Mahakama ya Mwanzo mjini hapa, mbele ya Hakimu
Jaffari Mkinga, mlalamikaji Asteria Mgabo anamtaka Yasinta amlipe Sh3
milioni baada ya kumfumania na mumewe wa ndoa aitwaye Martin Msangawale
(39), Mhasibu wa Manispaa ya Sumbawanga.
Siku hiyo ya kusikilizwa kwa shauri hilo
mlalamikaji katika shauri hilo Asteria anatarajiwa kuwaleta
mashahidi wake wanne mahakamani hapo
HABARI: SITTA KUGOMBEA URAIS 2015
Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta amesema
kwamba anazo sifa za kuwa Rais wa Tanzania na anafikiria kugombea 2015,
iwapo dhamira yake itaridhika na mazingira na upepo wa kisiasa wa wakati
huo.
Akizungumza katika mahojiano maalumu, Sitta alitaja mambo kadhaa aliyoeleza kuwa ni ishara ya
kukubalika kwake, ikiwamo kuteuliwa na marais wote wanne; Julius
Nyerere, Ali Hassan Mwinyi, Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete katika
nyadhifa mbalimbali ikiwamo ya uwaziri.
Kauli ya Sitta imekuja baada ya kuwapo kwa minong’ono ya baadhi ya wananchi kumtaja kuwa miongoni mwa watu wanaoweza kujitokeza kugombea urais katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2015.
Kauli ya Sitta imekuja baada ya kuwapo kwa minong’ono ya baadhi ya wananchi kumtaja kuwa miongoni mwa watu wanaoweza kujitokeza kugombea urais katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2015.
“Ni faraja kusikia watu wakinizungumzia kuwa
ninazo sifa (za kuwa Rais). Nami ninaamini ninazo sifa. Wakati
utakapofika nitajipima. Kama hali hii itaendelea, basi nitaona ni vizuri
nigombee,” alisema Sitta ambaye aliwahi kuwa Spika wa
BURUDANI: MH. JERRY SLAA MGENI RASMI USIKU WA MASTAA WA FILAMU
Meya wa Ilala Jerry Slaa ndiye
atakuwa mgeni rasmi kesho katika Tamasha la Usiku wa Mastaa wa Filamu
litakalofanyika katika ukumbi wa kisasa wa burudani Dar Live, Mbagala
Zakhem jijini Dar es Salaam. Katika tamasha hilo burudani mbalimbali
kutoka kwa wasanii wa filamu na wale wa Bongo Fleva zitakuwepo
HABARI: JESHI KUCHUKUA UONGOZI UGANDA?
Baada ya sakata la kufariki ghafla mbunge wa chama tawala NRM nchini
Uganda,rais Museveni pamoja na waziri wa ulinzi na mkuu wa majeshi
wamekuwa wakitoa kauli za kutishia kuliachia jeshi lichukue uongozi
nchini humo.
Subscribe to:
Posts (Atom)