Mapigano baina ya wanajeshi wa serikali ya Mali na wapiganaji wa
Kiislamu kwa mara ya kwanza yamefika kati-kati ya mji wa Gao, mji mkubwa
kabisa kaskazini mwa nchi.
Anasema ghasia zilianza karibu na makao makuu ya polisi, lakini mapigano yametapakaa.
Wanajeshi wa Ufaransa na Mali waliukomboa mji huo mwezi uliopita.
Shirika la habari la Ufaransa linaeleza kuwa wapiganaji wa Kiislamu waliovaa nguo nyeusi, huku wamebeba bunduki, waliteka eneo la kati ya mji wa Gao, mji wenye wakaazi wengi kabisa kaskazini mwa Mali.
Wapiganaji hao walipambana na wanajeshi wa Mali leo jioni kwa zaidi ya saa mbili na walionekana wakiranda mitaani kwa pikipiki na wengine walikuwa juu ya mapaa karibu na makao makuu ya polisi.
Karibu na makao hayo wanajeshi wa Mali walitumia makombora na kupambana kwa risasi na washambuliaji ambao wanafikiriwa kuwa wafuasi wa kundi la MUJAO, linalodai kupigana jihadi Afrika Magharibi.
Sauti zilizosikika ni risasi na mbuzi wakikimbia huku wakaazi wa mji wamejificha majumbwani mwao.
Tangu wanajeshi wa Ufaransa kuukomboa mji wa Gao, wapiganaji wa Kiislamu walipambana na wanajeshi nje ya mji lakini hii ndio mara ya kwanza wamefanikiwa kuingia ndani ya mji.
No comments:
Post a Comment